GEITA:CHADEMA YAWAFUKUZA UANACHAMA VIONGOZI WAWILI

Share it:



Image result for chadema


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoani Geita kimewafukuza na kuwavua uanachama viongozi wawili huku kikitoa onyo kwa wanachama wake kwa kuhusishwa na kashifa ya usaliti na kuhujumu Chama hicho.
Katibu wa Chadema Jimbo la Geita mjini   Kangeta Ismail amesema wanachama wake waliofukuzwa ni Edward Manyika ambaye alikuwa katibu mwenezi wa jimbo hilo na Daud Sunzu aliyekuwa mgombea Udiwani kata ya Kalangalala katika uchaguzi mkuu uliopita.

Amesema kufukuzwa kwa wanachama hao kumetokana na maamuzi ya kamati tendaji kupitia kikao cha dharura kilichoketi jana na kwamba wengine watatu wamepangiwa tarehe ya kuwasilisha utetezi wao

Kangeta ameendelea kusisitiza kwamba  chama hicho kitaendelea kuwachukulia hatua viongozi na wanachama wanaokiuka maadili ya Chama ambayo yamewekwa .  



Share it:

JOEL MADUKA

SIASA

Post A Comment:

Also Read

MAHAKAMA YAIKEMEA JAMHURI KUSHINDWA KUMPELEKA SETHI MUHIMBILI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeukemea upande wa Jamhuri kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumpeleka  mshtakiw

JOEL MADUKA