HONDWA MATHIAS AISIMAMISHA MWANZA

Share it:
Wananchi waliofika katika uzinduzi wa albamu ya nani kama mama ya Hondwa Mathias wakifatilia kwa makini burudani zilizokuwa zikiendelea katika viwanja vya ccm kirumba jijini Mwanza.

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini kutoka Dar es Salaam,Ikupa Mwambeja akiwa sambamba na Emmanuel Mgaya(Masanja) na Moses Mkoko wakiimba kwa pamoja wilmbo husemao adonai.

Ambwene Mwasongwe akiimba wimbo wa misuli ya imani pamoja na masanja katika uzinduzi wa Hondwa Mathias.

Ambwene Mwasongwe Akiwapagawisha mashabiki wake katika uwanja wa ccm kirumba jijini Mwanza.



Mshehereshaji wa shughuli hiyo Masanja Mkandamizaji akizungumza na waimbaji Bahati Bukuku,Ambwene na Christophe Mwangila,kuhusu kuchangia 

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi Emmy Mshana akisoma Risala mbele ya mgeni Rasmi.


Hondwa Mathias akiimba nyimbo iliyobeba albamu ya nani kama mama kwenye viwanja vya ccm Kirumba.


Mwandishi wa madukaonline blog,akizungumza na mratibu wa tamasha la uzinduzi huo,Peter Abdallah kujua kilichotokea kwenye tamamsha hilo.

Bahati Bukuku akiwa jukwaani.

Manonga classic mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka mwanza akiwa jukwaani.


Mwandishi wa Blog Promovertz,Jacktani Msafiri akichukua matukio ya picha katika uzinduzi huo.

Chirstopher Mwangila akiimba wimbo wa Mungu ni Mungu.

Kundi la waimbaji kutoka mwanza kihayile group wakiongozwa na Vannesa Laban jukwaani.

Wadau wakiwa katika mapozi wakifatilia kwa umakini tukio la uzinduzi.



Emmanuel Mwakisepe akiwa katika shahuku ya hali ya juu iliyopelekea kuwafuata watazamaji.



MWANZA:Serikali ya halmashauri ya wilaya ya Ilemala jijini Mwanza imeahidi kuendelea kuwasaidia watoto yatima na wajane pamoja na kuwahamasisha wadau mbalimbali kuendelea kutoa misaadaHayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya hiyo,John Wanga,mapema jana katika tamasha la kusaidia watoto yatima na wajane lilioenda sambamba na uzinduzi wa album ya mwimbaji wa nyimbo za injili Hondwa Mathiasi.

Wanga,amesema yeye pamoja na serikali wilayani Ilemela  itaendelea kuunga jitihada za wadau ambao wamekuwa wakiguswa na kujitokeza kwa kutoa misaada kwaajili ya watoto yatima pamoja na wakina mama wajane kwani inafahamika kuwa dini safi ni ile ambayo Inawajali yatima na wajane.“Niwaombe watanzania na wadau wote kwa ujumla muwe ni watu wa kuguswa kuwasapoti watu ambao wamekuwa na mahitaji hususani yatima na wajane kama ambavyo leo tumeona amefanya Hondwa Mathias”Alisema Wanga 

Aidha kwa upande wake mratibu  wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi huo,Peter Abdallah,Ameelezea Lengo la kuandaa tamasha hilo wamelenga kuwasaidia watoto yatima na wajane baada ya pesa ambayo itapatikana katika tamasha hilo.

“Lengo la kuandaa tamasha hili ni kusudio la kuona sisi tunasapoti watoto yatima na wajane na pia kurudisha fadhira kwaajili ya jamii ambayo ina uhitaji”alifafanua Peter.

Hata hivyo kwa upande wake Hondwa Mathias ,amefafanua kuwa kutoa msaada wa yatima na wajane ni kutokana na changamoto ambazo alikuwa akizipitia  wakati akiwa bado hajaingia katika tasinia ya uimbaji wa nyimbo za injili hali hiyo ndio iliweza kumsababisha kuguswa na kuamua kufanya tamasha na uzinduzi ambao utawashika mkono watu hao ambao wana uhitaji.

“Kwa sababu mimi nimepitia maisha magumu sana mimi nina wazazi lakini nilikuwa ninaona yatima na wajane wanavyoishi maisha ya ajabu hivyo swala hilo likanigusa na ndio maana nimeamua kufanya tamasha hili ambalo litatoa msaada kwa watu hawa”alisema Hondwa.

Vitu ambavyo vinatarajia kupelekwa kwa watu hawa wenye uhitaji ni chakula,mavazi na maradhi ikiwemo pesa kwa ajili ya kukidhi kituo ambacho kitapelekewa msaada huo.


Share it:

habari

mastaa

Post A Comment: