 |
Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu
Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa
Mradi wa Uoneshaji Filamu bure kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa
niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nnauye. |
 |
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania, Bi.Joyce Fessoo, akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye
uzinduzi huo ambapo aliwahakikishia Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na
nchini kwa ujumla kwamba Serikali itahakikisha inaboresha zaidi sanaa
ya filamu ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hiyo
ili filamu zinazozalishwa ziwe na ubora |
 |
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali
Mstaafu, Ezekiel Kyunga, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Uoneshaji wa
Filamu mkoani Geita, ambapo alisisitiza kwamba sanaa ni ajira hivyo
wanatasnia hiyo watumie fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo yanayotolewa na
serikali ili kuboresha zaidi kazi zao. |
 |
Katibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu
Zanzibar ZIFF, Robert Manondolo, akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo
alibainisha kwamba ZIFF imekuwa ikitoa ufadhiri kwa taasisi mbalimbali
nchini ikiwemo Taasisi ya Kijani Consult kwa lengo la kuziwezesha
kufikisha elimu kwa umma kwa njia ya kuonesha filamu bure na kufikisha
elimu iliyokusudiwa. |
Mkuu wa idara ya Habari, Kijani Consult
Tanzania, Rose Mweko, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa mradi wa
kuonesha filamu bure katika maeneo ya wazi mkoani Geita.
Katibu Tawala Wilayani Geita, Thomas
Dimme, akizungumza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu
bure mkoani Geita ili kufikisha elimu mbalimbali ikiwemo Ufugaji na
utunzaji wa Mazingira.
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika
Ukumbi wa Desire Park Geita ambapo Taasisi ya Sanaa Na Mazingira ya
Kijani Consult Tanzania imeanzisha kampeni ya kuonesha bure Filamu
mbalimbali kwa ajili ya kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya
Utunzaji wa Mazingira (Mabadiliko ya Tabianchi), Ufugaji wa kuku wa
kienyeji, Usalama barabarani, Madawa ya kulevya, Madhara ya ndoa za
utotoni miongoni mwa mambo mengi ya kijamii. Mradi huo umefadhiriwa na ZIFF.
Kutokana na Mwitikio wa wanatasnia ya
Filamu mkoani Geita kuonesha shauku ya kuwa na Maonesho hayo ya Filamu,
Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika
mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20
tangu kuanzishwa ZIFF.
Post A Comment: