WATU WATATU WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA WIZI WA PIKIPIKI KAHAMA

Share it:
Wananchi wakiwa katika makazi ya mtuhumiwa aliyechomwa moto wakishuhudia nyumba ikiteketea.
Shimo ambalo mtuhumiwa inadaiwa alificha pikipiki tatu ndani yake.
Wananchi wakiendelea kubomoa nyumba ya mtuhumiwa
Maafisa wa polisi wakiwa wameifikisha miili ya watuhumiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.


Wananchi waliojichukulia sheria mkononi jana  wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa pikipiki.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yalifanywa majira ya saa nane usiku wa kuamkia jana baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa jana  majira ya saa nne asubuhi.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake wawili waliouawa jana baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki tatu zimehifadhiwa kwenye shimo.

Afisa mtendaji wa mtaa wa Kitwana, Peter Joseph amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichulia sheria mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.

Miili ya marehemu hao ilichukuliwa na Jeshi la polisi wilaya ya Kahama, na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama

Share it:

JOEL MADUKA

matukio

Post A Comment:

Also Read

WAZIRI JAFO AAGIZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BWANGA UKAMILIKE NDANI YA MWEZI MMOJA

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi

JOEL MADUKA