Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni mpya za uchimbaji halikadhalika leseni ambazo zimeisha muda wake.
Mhe. Rais Magufuli amezungumzia uamuzi wa Serikali kupeleka Miswada Mitatu ya dharura Bungeni kuwa unatokana na umuhimu wa hilo katika kutetea maslahi mapana ya nchi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi.
Mhe. Rais Magufuli
amewaonya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wenye nia ya kugombea nafasi
mbalimbali katika Uchaguzi wa Chama hicho kutojihusisha na rushwa kwa vile
rushwa ni adui wa haki, hivyo, atakayebainika kutumia rushwa atapoteza sifa ya
kuwa Mgombea.
Akizungunzia ujenzi wa
barabara ya kutoka Kamanga hadi Sengerama kwa kiwango cha lami, Mhe. Rais Dkt.
Magufuli amesema kwa sasa Serikali imeshampata mkandarasi kwa ajili ya kufanya
upembuzi yakinifu na usanifu ili barabara hiyo ianze kujengwa katika kutimiza
ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Rais Magufuli pia amewataka
Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchni kufafanua kwa wananchi na kusimamia uamuzi wa
Serikali wa kufuta tozo zaidi ya 80 katika mazazo ya Kilimo, tozo 7 za Mifugo
na tozo 5 za Uvuvi ambao lengo lake ni kuwaondolea kero wananchi.
Aidha, amesema Serikali
inafanya uchambuzi ili kubaini wale wote waliotoa pembejeo hewa na
atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Wakati huo huo, Mheshimiwa
Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha utoaji wa leseni
mpya za uchimbaji na halikadhalika leseni ambazo zimeisha muda wake. Ametoa
maagizo hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Geita ambao walizuia msafara
wake katika maeneo mbalimbali wakati akiwa njiani kuelekea Chato.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Sengerema,Mwanza
04 Julai 2017.
Post A Comment: