Baadhi ya Wakurugenzi Kutoka Kwenye Halmashauri Zilizopo Kwenye Mkoa wa Geita wakifuatilia Kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini -TASAF awamu ya Tatu. |
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Geita Harun Elikana akiwasilisha Taarifa ya Shughuli ambazo zimekwisha kufanyika kwenye Mkoa huo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Kikao hicho Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwahutubia wajumbe wakati wa ufunguzi wa kikao hicho. |
Wakuu wa Wilaya ya Bukombe na Mbongwe wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi. |
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Waratibu wa TASAF Mkoani Geita wamekutana kwenye Kikao cha tathimini ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF AWAMU YA TATU).
Lengo likiwa ni kufanya Tathimini ya utekelezaji wa shughuli za TASAF tangu Julai ,2015 hadi sasa.
Akifungua Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,amesema kuwa katika ufuatiliaji ambao ameufanya kwenye Halmashauri zote na kufanya mikutano na Walengwa pamoja na viongozi katika vijiji vyao,amebaini kuna malalamiko kadhaa kutoka kwa walengwa ambayo yanaitaji kushughulikiwa.
"Pamoja na kuwepo kwa malalamiko pia kuna nimeona mabadiliko ya kimafanikio kwa kaya mbali mbali nilizozitembelea ,kwa kweli matunda ya mpango yanaonekana kwa walengwa walio wengi kwa mfano nilifurahishwa sana nilipotembelea kijiji cha Mwalo Wilaya ya Bukombe ambapo viongozi wa kijiji na walengwa wa mpango wamejiwekea utaratibu kwamba wakati wanaendelea kutimiza masharti ya Elimu na afya matarajio yao ni kuona kila mlengwa anajenga nyumba na kuezeka kwa bati"Alisema Kyunga.
Kyunga ameongeza kuwa Wilaya ya Chato ndiyo ilikuwa inashika nafasi ya kwanza kitaifa kwa kuwa na walengwa wengi ambao wamehamasika na kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF)ambapo Kaya 7,250 kati ya Kaya 8,046 zilikuwa zimekwisha jiunga na mfuko huo.
Aidha Amewataka na wasimamizi wa mpango wa TASAF awanu ya Tatu ngazi ya Vijijini/Mitaa kufuatilia kaya ambazo zimenufaika na mfuko wa kunusuru Kaya Masikini
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Post A Comment: