Mwenge wa Uhuru ukiingia kwenye viwanja vya Nyamadoke Wilayani Sengerema ambapo ndipo ambapo yalifanyika makabidhiano ya Kimkoa kati ya Geita na Mwanza. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour akishukuru na kuwaaga viongozi wa Mkoa wa Geita kwaajili ya majukumu ya kukimbiza mwenge kwenye Mkoa wa Mwanza. |
Viongozi wa Mkoa wa Geita wakiimba wimbo wa Geita. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu ambaye pia alikuwepo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. |
Mkuu wa Wilaya ya Magu akipokea mwenge wa uhuru kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa makabidhiano ya kimkoa. |
Mkuu wa wilaya ya Magu Hadija Nyembo akisoma taarifa na shughuli ambazo zitafanywa na mwenge wa uhuru kwenye Mkoa wa mwanza. |
Mbio za
Mwenge wa Uhuru zimemalizika Mkoani Geita huku kukionekana baadhi ya miradi ya
serikali kuwa na mapungufu mengi kuliko ya watu au sekta binafsi ambayo imekuwa
ikizinduliwa na kuwekewa Mawe ya Msingi.
Hayo
yamebainishwa na Frederick Joseph Ndahani Mkimbiza Mwenge wa Uhuru
Kitaifa,Wakati alipokuwa akitoa salamu za mwenge wa Uhuru Wilayani Geita, amesema
kuwa miradi ya serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kuliko ya binafsi na bado
inakuwa na mapungufu ambayo yamekuwa yakisababisha miradi hiyo kutokuzinduliwa.
Ameendelea
kuongeza kuwa tatizo kubwa ambalo linasababisha miradi ya serikali kuwa mibovu
ni kutokana na baadhi ya viongozi kutokuwa waaminifu na kujikuta wakitumia
mwanya huo kujilimbikizia mali huku wakiacha miradi ya serikali ikiharibika
kabla ya muda.
Akikabidhi
mwenge wa Uhuru kwenye Mkoa wa Mwanza,Wilayani Sengerema,kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa huo,Mkuu wa Wilaya ya Geita,MwL,Herman Kapufi ameelezea kuwa kati ya miradi
sabini na mbili (72) ambayo imepitiwa na mbio za mwenge wa uhuru miradi miwili (2)
haikufanyiwa kazi kutokana na kutokukidhi vigezo vya kuzinduliwa na kwamba yale
makosa ambayo wameambiwa kurekebisha watahakikisha wanarekeshibisha.
Mbunge wa
Jimbo la Geita Mjini,Constantine Kanyasu amesema kuwa tatizo lipo kwenye
usimamizi kwa kumkabidhi mkandarasi bila
ya kufuatilia Miradi husika na kumwamini kuwa anaweza kufanya bila ya kukosea
kwenye swala la ujenzi.
wa
uhuru umemaliza kuzindua,kutembelea na kuweka mawe ya msingi Kwenye Halmashauri
sita zilizopo Mkoani Geita na kukabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Magu
Bi,Khadija Nyembo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu Wilaya ya Geita,Mwl Hermani Kapufi kwa Niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Geita makabidhiano ambayo yamefanyika kwenye Kijiji cha Nyamadoke,Jimbo
la Buchosa Wilaya ya Sengerema.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: