Frederick Joseph Ndahani Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, wakati akizunguza na hadhara ya wananchi |
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ,Amour Hamad Amour akiweka Jiwel la Msingi kwenye Mabweni ya shule ya Sekondari ya Nyachiluluma |
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ,Amour Hamad Amour,akikagua Bweni la wasichana la shule ya Sekondari Nyachiluluma |
Wazazi,Walimu
na Jamii imetakiwa kuwajengea Watoto pamoja na wanafunzi ambao wapo shule za
Msingi na Sekondari misingi ya maadili na uzalendo katika ufundishaji wa Masomo
na malezi pindi wanapokuwa Nyumbani ili
kuweza kuwasaidia kuwa na moyo wa kulipenda Taifa na kulinda rasilimali zilizopo Nchini.
Rai
hiyo imetolewa na Frederick Joseph Ndahani
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, wakati akizunguza na hadhara ya wananchi,
wanafunzi pamoja na walimu wa sekondari
ya Busanda iliyopo Kata ya Busanda katika
Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Ndahani,
amesema kama wanafunzi watajengwa katika Misingi iliyo imara hapo badae,
watakuwa viongozi bora wenye kusimamia
ukweli katika shughuli za ujenzi wa taifa.
“Tunatambua
kwamba watoto hawa wakijengewa msingi imara ndio wanaweza kuja kuwa mabarozi
wazuri wa kupinga vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikiathiri kwa kiasi kikubwa
pato la Taifa na kuwanyima watu haki “Alisisitiza Ndahani
Awali
akizindua Bweni la wanafunzi wa kike
katika Sekondari ya Nyachiluluma lililogharimu fedha za Wananchi,
halmashauri na serikali kuu zaidi ya Sh. Milioni 130, Kiongozi wa mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour amewasisitiza wanafunzi wa kike
kutumia nafasi hiyo ambayo serikali imeona ni vyema kuweka mabweni kwa kusoma
kwa bidii na kuachana na mambo ambayo yanaweza kuwasababisha kutokutimiza
malengo yao.
Kwa
Upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari
Nyachiluluma Richard Musiba amesema mwaka wa jana Wanafuzi watatu walibainika
kuwa na ujauzito na mwaka huu ni wanafunzi wawili na wote
wamekwisha ondolewa shuleni.
Post A Comment: