Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru ,Amour Hamad Amour pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi wakikagua mtambo wa kuchakata Alizeti. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru ,Amour Hamad Amour akiweka Mbigu za Alizeti kwenye mashine ya kuchakata. |
Ubao unaonesha kikundi kilipo. |
Wnanchi wakifuatilia zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye kiwanda kidogo cha kuchakata alizeti. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru ,Amour Hamad Amour akiweka Jiwe la Msingi kwenye Kiwanda kigodo cha kuchakata alizeti |
Vikundi vya wajasiriamali Wadogo wadogo bado vinakabiliwa na
changamoto mbali mbali likiwemo swala la kukosekana kwa vifungashio vya bidhaa
ambazo wamekuwa wakizitengeneza kwaajili ya kuingiza Sokoni Hali ambayo
inapelekea kushuka kwa thamani Bidhaa ambazo wanaingiza Sokoni.
Hayo yametokea wakati wa uzinduzi wa mradi wa kukamua na kusindika
mafuta ya alizeti cha Chemamba wilayani Geita ambapo wanakikundi cha
ujasiriamali wamekuwa wakikusanya chupa ambazo zimekwisha kutumika na kuwekea
mafuta na pia rebo wamekuwa wakitumia kwa kuandika kwa Mkono na sio zile ambazo
zinakuwa zinatambulisha shughuli za kikundi pamoja na namba za simu za
wahusika.
Kutokana na hali ambayo wamekutwa nayo wanakikundi hao na Kiongozi
wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad
Amour imemlazimu kuagiza Halmashauri husika kukikopesha kikundi hicho fedha
ambazo zitawasaidia katika kuboresha shughuli ambazo wanazifanya.
Akisoma risala na taarifa ya Mradi Huo kwa Kiongozi wa mbio za mwenge uhuru Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya
Geita Jeremia Kengere amesema uwepo wa mradi huo umehamasisha
wananchi kujikita kulima zao hilo la alizeti kwani wengi wao wamenufaika
kutokana na kilimo hicho.
Mkuu wa Wilaya hiyo,Mwl Herman
Kapufi ameitaka halmashauri husika kuhakikisha wanakipa kipa umbele kikundi
hicho kwa kukiwezesha Mkopo ambao utawasaidia kujikwamua Hali ambayo wanayo
kwasasa.
Mwenge wa uhuru
umezindua na kutembelea na kuweka jiwe
la msingi miradi Kumi Na Moja na kukibizwa wilaya ya Nyangh'wale.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: