|
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhueu Kitaifa,Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi wakati wa kukimbiza mbio za mwenge kwenye Wilaya ya Geita. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi. |
|
Mwenge wa Uhuru ukipitishwa kwenye kamati ya Ulinzi na usalama Wilayani Geita. |
|
Mwenge wa Uhuru ukipitishwa kwa viongozi wa Dini na madhahebu mbali mbali Wilayani Geita. |
|
Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencian Bukwimba akizungumza na kutoa salaam Kwa wananchi wa kijiji Nyachiruruma. |
|
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akiweka Jiwa la Msingi kwenye Kituo cha afya cha Inyara. |
|
Vitanda ambavyo vimo kwenye kituo hicho. |
|
Mradi wa Green House ambao unasimamiwa na kikundi cha viajana wa Busanda. |
|
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Wilaya na Mkoa wa Geita wakitembelea Mradi wa Kilimo cha Green House. |
|
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa,akimpongeza Diwani wa Kata ya Busanda Elias Kisome kwa shughuli ya kuwajengea vijana uwezo wa kulima kilimo hicho. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi pamoja na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Thomas Dimme wakimsikiliza Kiongozi wa Mwenge wa uhuru Taifa.
Vijana wametakiwa kujiajili kwa kuunda vikundi ambavyo vinaweza
kuwasaidia kupatiwa Mkopo kutoka kwenye Halmashauri ambazo wanaishi.
Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour wakati alipokagua kikundi cha vijana
ambao wanajishughulisha na kilimo cha Green House Kwenye kata ya Busanda
Wilayani Geita.
Amesema kuwa Vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo
ni vyema wakawezeshwa kwa Mikopo ikiwa ni pamoja na kufuatiliwa kwa kina miradi
ambayo wanakuwa wameianzisha.
Pia ameongeza kuwa kukaa pamoja ni jambo
ambalo linaweza kuchukua muda lakini ni jambo zuri kwani palipo na umoja kuna
nguvu kubwa ya mafanikio.
“Hatuitaji viongozi ambao hawapo tayari
kuwasaidia wananchi nyie niwapongezeni nakijua kilimo cha green house nina
amini kuwa mtapata faida kwa kile ambacho mmekitumia kinaweza kurudi mala mbili
zaidi”Alisema Hamad
Japhet Msuka,ameeleza kuwa kilimo ambacho
wamekuwa wakikifanya kimeweza kuwaletea maendeleo ya vipato vya kuendeleza
maisha pamoja na kukidhi haja zao.
Hata hivyo Kiongozi wa mbio za Mwenge Amour
Hamad Amour pamoja na Kuwapongeza wanakikundi hicho ambacho kinavijana Arobaini
na Mbili pia amempongeza Diwani wa kata hiyo, Elias Kisome kwa juhudi ambazo amezifanya hadi
kufikia hatua ya kuwakusanya vijana na kuwapa mbinu ya kubuni mradi huo.
|
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: