Wakimbiza mwenge Kitaifa wakikagua Soko la Namonge. |
Soko la Mazao la Namonge |
Kiongozi wa mbio za mwenge akikagua baadhi ya mabanda kwenye Soko la nafaka la Namonge. |
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akionesha eneo la ukuta wa Ghara kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Amour Hamad Amour akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya Bukombe Chacha Moseti. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Amour Hamad Amour Akizindua Soko la Mazao baada ya kuwa ametoa maelekezo ya ukarabati wa soko hilo.
PICHA NA JOEL MADUKA(MADUKA ONLINE)
|
Kiongozi wa
mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour
Hamad Amour amesikitishwa na Ujenzi wa mradi wa soko la Mazao Namonge lililopo wilayani Bukombe Mkoani Geita kwa kujengwa chini ya kiwango na hali ambayo
imepelekea kuwepo kwa nyufa nyingi kwenye maeneo mengi ya jingo hilo.
Na pia amemtaka mkandarasi kurekebisha haraka iwezekanavyo kabla ya mwenge wa uhuru kuondoka Mkoani humo huku akimpa siku mbili maeneo yote ambayo yananyufa kufanyiwa ukarabati haraka zaidi.
Kiongozi huyo wa mwenge ameendelea kuwasisitiza viongozi wa halmashauri kuhakikisha wakandarasi wanakuwepo katika miradi inayozinduliwa,kuwekewa jiwe la msingi na kutembelewa na mwenge wa uhuru ili kujibu changamoto zitokanazo na miradi hiyo.
Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo CHACHA MOSETI ametoa taarifa ya mradi huo kwa mwenge na gharama Sh,581,217,690 hadi kukamilika kwake ambapo Sh,552,156,805.5 ni Fedha za serikali kuu kupitia mpango wa market insfrastructure,value addition and Rural Finance na Sh,29,060.884.5 ni mchango wa Halmashauri.
Aidha mpaka sasa jumla ya fedha zilizotumika ni Sh ,552,156.805.5 ambazo ni fedha za serikali kuu.
Hata hivyo Baada ya kukagua maeneo mbalimbali ya soko hilo na kujionea ujenzi huo Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa AMOUR HAMAD AMOUR akatoa maagizo.
“Baada ya kukagua mradi huu tumeona mapungufu mengi mradi umepasuka kwenye kuta sasa kwa vile mradi huu umekusudiwa kuwekewa jiwe la msingi na tumemuuliza mkanadarsi hayupo eneo husika wakandarasi wanatakiwa kuwepo kwenye mradi ili kujibu maswali ambayo yatakuwa yakiulizwa Tunamuomba mkandarasi kabla ya risala ya utii kwa
Mheshimiwa Rais awe amefika uwanjano na tunatoa siku mbili awe amekamilisha ukarabati wa kasoro ambazo tumezikuta “Alisisitiza Hamad.
Wafanyabiashara wa zao hilo Mlalu Bundala na Emmanuel Mhuli Kasuku wamezungumzia umuhimu wa soko hilo litakapokamilika kuwa litawasaidia kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya zao ambalo wanalilima.
Kauli mbiu ya mwenge huu ni "Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu."
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Post A Comment: