![]() |
Vijana therasini ambao ni Raia wa nchi ya Burundi wakiwa wameshikiliwa na Idara ya uhamiaji Mkoani Geita Kabla ya kufikishwa mahakamani. |
![]() |
Naibu kamishina wa idara ya uhamiaji Mkoani Geita, Wilfred Marwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. |
Idara ya uhamiaji Mkoani Geita imewakamata Raia wa
Burundi Therasini (30) ambao wanaishi na kufanya kazi Nchini kinyume cha sheria
na wengine wakikamatwa kwenye zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya Taifa
ambalo linaendelea Mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za uhamiaji
Mkoani humo,Naibu kamishina wa idara ya uhamiaji Mkoani Geita, Wilfred Marwa
amesema kati ya hao Raia kumi na nane ( 18) ambao wapo
nchini kinyume na sheria na wanafanya kazi mbalimbali za kujiingizia kipato na
wengine kumi na mbili (12) walikuwa
kwenye zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya Taifa jambo ambalo ni kinyume cha
sheria.
Naibu kamishina Marwa ametaja kazi ambazo wamekuwa
wakizifanya Raia hao wa kigeni kuwa ni kazi za kilimo na ufugaji.
“Mara nyingi watu hawa wanajishughulisha sanaa na
kazi za ufugaji wa Ng’ombe na kilimo cha
Mananasi pamba na mpunga kwenye maeneo ya vijijini”Alisema Marwa.
Aidha kwa upande wake moja kati ya Raia wa Burundi
aliyekamatwa na idara ya uhamiaji Bw,Kajoro Richard alisema sababu ambazo
zimekuwa zikisababisha kuingia nchini ni kutokana na ugumu wa maisha nchini
mwao na kukosekana kwa ajira.
“Mimi Kweli nilikuja hapa Tanzania nikitokea nchini
kwetu Burundi kwa sababu ya kuja kutafuta maisha kwetu ajira ni ngumu sanaa ila
naomba wanisamehe nipo tayari kurudi nchini kwetu”Alisema Kajoro.
Naibu kamishina Wilfred Marwa amesema zoezi hilo ni
endelevu na kwamba amewataka raia wa kigeni kufuata utaratibu kwa kufuata
vibari vya kukaa nchini kwa njia ya halali huku akiwataka watanzania ambao
wanaishi na Raia hao kuachana na tabia hiyo na kwamba watakamatwa watafungwa
kifungo cha miaka 20 au faini ya milioni
ishirini 20.
Post A Comment: