Mratibu msaidizi wa afya ya uzazi Mkoani Geita,Bi Mbeleje Donald akitoa maelekezo ya namna ambavyo watoa huduma wanatakiwa kuzingatia wakati wa zoezi la Chanjo ya mlango wa uzazi.
Mkoa wa Geita unatarajia kuanza zoezi la chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa
Wasichana wenye Umri wa miaka kumi na nne(14) lengo likiwa ni kuwakinga na
maambukizi ya virusi vya human papilloma.
Saratani ya Mlango wa kizazi imekuwa ikiongezeka
kila mwaka kwa nchi na takribani watu
elfu hamsini wamekuwa wakiongezeka na
kusababisha vifo vya wakina mama wengi pamojana na mabinti.
Akizungumza na wadau wa sekta ya afya Mkoani Humo,Mkuu
wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel ametaja sababu ambazo zimeendelea
kusababisha saratani ya mlango wa kizazi
ni pamoja na kujamiiana kwenye umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi ndoa za mitaara pamoja na uvutaji wa sigara.
“Ndugu washiriki
kuna dalili ambazo zinaweza kusababisha ugonjwa wa saratani Kuto kwa
damu bila mpangilio au kutokwa damu baada ya kujamiana Maumivu ya mgongo, miguu
na au kiuno Kuchoka, kupungua uzito, kupungikiwa hamu ya kula Kutokwa uchafu
uchafu kwenye uke wa majimaji, uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu Kuvimba
mguu mmoja”Alisema Robert.
Kwa upande wake Mratibu msaidizi wa Afya ya uzazi Mkoani
humo,Bi Mbeleje Dornad alisema kwa hapa nchini takribani wanawake laki nne na
sitini na tisa elfu wamegundulika na maambukizi ya saratani ya mlango wa
kizazi.
“Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake
466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi, na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea”Alisema
Bi,Mbeleje.
Kaimu Mganga mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita,Joseph
Odero amewataka wazazi pamoja na walenzi kutoa ushirikiano pindi zoezi hilo
litakapo anza tarehe 23 mwezi huu wa aprili hikiwa ni pamoja na kuwaruhusu
mabinti wenye umri wa miaka 14 kufanyiwa chanjo hiyo.
Takwimu kutoka hospitali ya Occean Road inaonyesha
kwamba, Saratani ya Mlango wa Kizai inachangia kwa asimilia 36 ya saratani
zote, Asilimia 70 ya wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi wanajitokeza
katika hatua ambayo tayari saratani imesha samba maeneo mengine mwilini.
|
Post A Comment: