Wakuu wa Wilaya zilizopo Mkoani Geita pamoja na wabunge na wadau wa Kilimo cha Pamba wakifuatilia kwa makini Mkutano huo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ,Dionis Myinga akijitambulisha mbele ya wadau wa sekta ya kilimo cha pamba. |
Wada wa Kilimo cha Pamba wakiwa kwenye Mkutano wa majadiliano ya kuboresha kilimo hicho. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo cha pamba |
Katibu tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita ambaye pia anahusika na maswala ya Kilimo,Emmly Kasagara akitoa taarifa ya Kilimo cha pamba Mkoani humo. |
Zao la
biashara la pamba ni moja kati ya muhimili mkubwa wa uchumi nchini na katika
Mkoa wa Geita lakini kwa miaka ya hivi karibuni limeendelea kupoteza umaarufu kutokana
na mbegu kutokuwa na ubora pamoja na viuatilifu na bei kutokuwa na mpangilio.
Hali hii
ndio inayosababisha wadau wa pamba wakiwemo Viongozi wa Wilaya,Wabunge ,maafisa
Kilimo,washauri na wakulima kukutana kwenye ukumbi wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa
Geita kujadili namna wanavyoweza kuendelea kuinua kilimo cha pamba ili kuwa na
faida kwa mkulima na mnunuzi.
Katika
Mkutano huo Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga amesisitiza kwa wadau wa kilimo cha pamba kuwa kila mmoja
anawajibu wa kuhakikisha kuwa kilimo hicho kinarudi na kinafufuliwa katika
ubora wake uliokuwepo miaka ya nyuma.
“Tunawajibu
wa kuhakikisha kwamba kilimo hiki kinarudi kwenye ubora wake na hakuna
kinachoshindikana ni sisi kujipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kurejea historia
kwani itatusaidia”Alisema Kyunga.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe,Safari Nicas Mayala,ameelezea sababu za zao
la pamba kuanguka ni kukosa mtu anayeweza kuhudumia na kwamba zamani vyama vya
ushirika vilikuwa makini katika usambazaji wa mbegu zenye uhakika.
“Pamba
imeanguka baada ya kukosa mtu wa kuihudumia, mtu wa kuhihudumia alikuwa ni
ushirika vyama vya ushirika hadi miaka ya 1990, sasa hivi wangekuwa wamesambaza
mbegu ya pamba na dawa na Siyodani na ndio maana hapa mkulima amesema kwamba
turudishie Siyodani namba 25 ilikuwa inafanya kazi vizuri licha ya kupingwa
marufuku kutokana na uharibifu wa mazingira”Alisisitiza Mayala.
Akifunga
Mkutano huo Mkuu wa Mkoa Ezekiel Kyunga,amesisitiza kuwa suala la umoja wa wanunuzi
wa zao la Pamba, UMWAPA halipo kwani walipatiwa ridhaa ya mwaka mmoja kama
majaribio na Waziri ambaye alikuwa madarakani kwa miaka hiyo na kwamba
walipatiwa wafanye kazi kwa majaribio kwa mwaka mmoja na wameshapatiwa maelekezo ya kutowakandamiza
wakulima kupitia UMWAPA.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
Post A Comment: