Mradi wa usambazaji wa maji ambao upo kijiji cha Kilimani |
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour,akiweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa maji |
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour,amewataka Watanzania kujenga desturi ya kupenda kununua Bidhaa ambazo zinatengenezwa na kuzalishwa hapa Nchini kwaajili ya kuendelea kuwanyanyua wajasiriamali wadogo pamoja na kuinua kipato cha Nchi
Rai hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizindua klabu ya mapambano dhidi ya ukimwi kwenye shule ya Sekondari ya Zhakia Meghji iliyopo Wilayani Chato Mkoani Geita,amesema kuwa Mikakati ya serikali ya kuhakikisha kwamba wanakuza uchumi wa Taifa haitawezekana endapo kama watanzania awatajari bidhaa ambazo zinatoka nchini Hapa.
Aidha Amour ameendelea kusema kuwa katika kuhakikisha nchi inakuwa ni ya maendeleo ni lazima kuwepo kwa mikakati thabiti ya kupambana na mambo ambayo yamekuwa yakirudisha Nyuma maendeleo likiwemo swala la uvivu,maradhi na vitendo ambavyo vinakiuka misingi ya Nchi.
Sanjali na
hayo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa ,ameweza kutembelea na kuweka
jiwe la Msingi kwenye mradi wa usambazaji maji ambao upo kwenye Kijiji cha
mlimani.
Akisoma
taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ,kaimu mhandisi wa maji kwenye Halmashauri hiyo Mali Msango
,amesema kuwa mradi huo umeanzishwa kwa lengo la kuwapatia maji safi na salama
na zaidi ya wananchi elfu ishirini na tano wananufaika na mradi huo.
Wakazi wa
Chato,Maria Malare na Richard Bagolele,wamesema kuwa kuwepo kwa mradi huo na
kuongezwa kwa Matanki imeleta msaada Mkubwa sana kwani walikuwa wakipata shida
hapo awali Tofauti na sasa.
Miradi
ambayo imepitiwa ni 12 na ambayo imezinduliwa ni saba,minne imetembelewa na mmoja utawekewa
jiwe la msingi ambapo miradi yote ina thamani ya shilingi
,2,042,896,037.50 kati ya fedha hizo wahisani wamechangia shilingi,1,255.611.875, serikali
kuu 691.808.162.50 halmashauri 91.020.00 na wananchi shilingi 4.456,000.
Post A Comment: