Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mustapha
Bapumia (62) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anashangaa
mtu mwenye umri mdogo kama Yusuf Manji (41) kuwa na vyuma vinne kwenye
moyo.
Alieleza kuwa na vyuma vinne kwenye moyo ni hatari na kwamba anatembea katika kamba nyembamba.
“Kitaaluma huyu ni lazima ajiangalie sana yupo katika hatari anaweza kupoteza maisha muda wowote.”
Dk
Bapumia ambaye ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi alimeeleza hayo
jana Jumatatu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa
ushahidi katika kesi inayomkabili Manji ya kutumia dawa za kulevya aina
ya Heroine.
Akiongozwa
na Wakili Hajra Mungula kutoa ushahidi, Dk Bapumia alisema yeye kwa
siku huwa anawaona wagonjwa 50 hadi 60 na kwamba Februari 21, 2017
ilikuwa ni mara ya kwanza Manji kupelekwa kwao akiwa na maumivu ya moyo.
Ameeleza
kuwa wana utaratibu wa wagonjwa tete kuwapeleka katika kitengo cha
dharura na kwamba Manji walimpokea, wakamlaza, wakamchunguza na kuona
ana tatizo sugu la moyo pamoja na kuwa na umri mdogo.
"Nikatafuatilia
historia na kubaini licha ya kuzibuliwa kwa mishipa yake mitatu India,
Dubai na Marekani, ilikuwa bado haijaziba lakini alikuwa bado anapata
maumivu ya moyo," ameeleza shahidi huyo.
Ameeleza
kuwa walimfanyia vipimo na vilionyesha tatizo lipo na kuna sehemu ya
nne inahitaji kuzibuliwa na kwamba mgonjwa alikuwa wazi kuwa anatumia
sigara na pombe.
Kutokana
na hali hiyo ameeleza walimshauri mgonjwa ili waweze kuzibuliwa lakini
akawaambia waache na akaomba dawa kwa kuwa familia yake ipo Marekani na
matibabu yake mengi yanafanyika huko.
Shahidi
huyo alieleza kuwa wao kama hospitali hawezi kufanya chochote bila
ridhaa ya mgonjwa hivyo wakampatia dawa na akaruhusiwa Februari 24,
2017.
Alieleza
kuwa siku hiyo hiyo alirejeshwa tena hospitalini hapo nyakati za saa
mbili usiku akisumbuliwa na maumivu kwenye moyo, wakamlaza mpaka tarehe
Machi 14, 2017 ambapo aliruhusiwa.
“Katika kipindi hicho Manji aliridhia na kuzibuliwa vyuma kwenye moyo.”
Ameeleza
kuwa walimpatia dawa ikiwamo za kupunguza kolestro (mafuta) kupunguza
maumivu sugu ya mgongo pamoja na kupunguza hofu ambazo zimo ndani ya Morphine na Benzodiazepines.
Kwa upande wake Manji akijitetea aliiomba Mahakama imuachie huru.
Akitoa
ushahidi wake alieleza kuwa yeye ana matatizo ya moyo ya kurithi kutoka
kwa babu zake ambao walikwishafariki kwa ugonjwa huo.
Ameeleza
kuwa ugonjwa wa moyo ulimuanza akiwa na umri wa miaka 26 na kwamba mara
nyingi amekuwa akitibiwa nje ya nchi ikiwamo India na Marekani na ana
vyuma vitano kwenye moyo.
Akitoa
ushahidi mahakamani hapo, Manji ameeleza kuwa kila baada ya miaka
miwili anavibadilisha na kufanya uchunguzi vinafanya kazi vipi.
Akiongozwa
na wakili wake, Hajra Mungula, Manji ameeleza kuwa katika ripoti zake
za kati ya 2009 na 2016 haijawahi kutokea akaonekana kama anatumia dawa
za kulevya.
Manji akiendelea kujitetea ameeleza kuwa anatumia vidonge 30 hadi 35 kwa siku.
Manji
ameeleza kuwa polisi walikuwa wastaarabu wanampatia dawa na kwa upande
wa Magereza vidonge vilikuwa katika kabati wanampatia.
Manji
ameeleza kuwa Februari 8, 2017 alipata taarifa ya kutuhumiwa utumiaji
wa dawa za kulevya na kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum
(ZCO).
Baada
ya kuipata taarifa hiyo ameeleza aliitisha mkutano na waandishi wa
habari kukanusha taarifa hiyo na Februari 9, 2017 alikwenda polisi kwa
sababu anaheshimu jamuhuri na alitaka kazi ifanyike kwa haraka.
Ameeleza
alivyokwenda alichukuliwa na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali
ambapo alikutana na Gwajima(Askofu Josephat) na akatoa sampuli ya mkojo.
Ameeleza kuwa baada ya hapo walikwenda kukagua nyumbani kwake walichukua kompyuta, credit card na visa card.
Amesema
kuwa anashangaa kwanini walichukua hivyo vitu wakati havihusiani na
kesi ya dawa za kulevya na kuliacha sanduku lililokuwa na sindano na
vifaa tiba.
Aliongeza
kuwa inajulikana kuwa kuna ugomvi wa kibiashara ambapo wanagombea
kampuni ya Tigo na kwamba hiyo kesi ni propaganda na ni mchezo mchafu.
Amesema hiyo kesi imemuathiri yeye binafsi na baba yake alimuachia vitu viwili jina zuri na maadili kwa jamii.
Pia
imemuaribia jina kwa jamii yake, msikitini anashindwa kwenda kusali,
biashara pia na imeumiza watoto na imemfanya aachie Uenyekiti wa Klabu
ya Yanga.
Amesema
kuwa kutokana na kesi hiyo anaona aibu kukaa na viongozi ambao
anafahamiana nao akiwamo Raila Odinga na rais mstaafu Benjamin Mkapa
Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo itakapoendelea kwa ushahidi wa upande wa utetezi.
Awali
Manji alidai kuwa yeye ni mshauri wa kampuni za familia na kwamba
alikataa tuhuma za dawa za kulevya ili mahakama imsikilize na kutenda
haki na kwamba dawa aina ya Morphine na Benzodiazepines ni sehemu ya
dawa zake ambazo anatumia.
CHANZO/MPEKUZI.
Post A Comment: