Kichaka ambacho kipo ndani ya ziwa Viktoria na baadhi ya mitumbwi ya wavuvi ambacho ndicho kinasadikika mamba huyo upenda kujificha kwenye maeneo hayo. |
Ramadhan Dadila ni moja kati ya watu ambao walikuwa na marehemu hapa anazungumza na waandishi wa habari namna ambavyo waliachana wakati wakiwa kwenye shughuli za uvuvi. |
Afisa mtendaji wa Kijiji hicho Bw,Beatus Mazezele akielezea namna ambavyo walipatiwa taarifa ya mtu huyo kushambuliwa na mamba . |
Wanakijiji wakiwa wamekusanyika kando kando ya vikwe wakisubilia kuanza kumuwinda Mamba . |
Mkazi wa Kata na kijiji cha Bukondo
Wilayani Geita Bw Yusufu Samson
amemezwa na mamba wakati akiwa katika
shughuli zake za uvuvi
Oktoba 2.
Maduka Online imefika
Kijijini Hapo na kuzungumza na Baadhi ya
watu ambao alikuwa nao katika shughuli hiyo ya uvuvi ambapo wameelezea
hali ilivyokuwa na hadi
umauti ulipomkuta, John Katamla
na Ramadhan Dadila,wameelezea kuwa
walikuwa naye wakati
wa shughuli za kuloa
samaki lakini hata hivyo hali haikuwa
nzuri hivyo ilibidi
wakunje ndoano kwa ajili ya
kurudi Nyumbani ingawa marehemu alikuwa
anaendelea kuvuta kamba
za nanga.
Mwenyekiti wa
Kijiji hicho MAKOYE
SOJINGWANONI amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema
asubuhi wamemwona mamba huyo akitembea maeneo hayo lakini hawakuweza
kumfanya lolote hivyo wameomba
msaada kutoka kwa
mali asili.
Mtendaji wa Kijiji cha Nyansalala,Bw Beatus Mazezele amesema
tukio la kukamatwa na mamba mtu sio la mara ya kwanza kwani yamekuwa ya kijirudia mara kwa
mara hata hivyo ametoa wito kwa
wananchi kuachana na dhana ya kuendelea kuogelea maeneo
ya ziwani.
Afisa
wanyamapori wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Msese Msese amesema
hadi kufikia siku ya jana walipata baadhi ya vipade vya mwili
na bado wanaendelea na jitihada ya
kuutafuta mwili huo pamoja na mamba
ambaye amekuwa ni tishio kwa wananchi wa maeneo hayo.
Post A Comment: