Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo Akizungumza na waandishi wa Habari juu ya tukio la kuandamana wa madiwani wa Halmashauri mbili za Mji na Wilaya.
Jeshi la polisi Mkoani Geita linamshikilia
Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Kasheku
Msukuma kutokana na tukio la maadamano ambayo yalifanyika siku ya Alhamisi wiki
hii yaliyopelekea uharibifu wa
miundombinu ya maji kwenye mgodi huo.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani
Geita,Mponjoli Mwabulambo amezungumza na Maduka online ambapo amesema kuwa wanawashikilia madiwani
sita pamoja na mbunge huyo kwaajili ya
kufanya nao mahojiano ambayo yatabaini ni wakina nani ambao wamehusika na tukio
hilo la kuandamana kinyume na sheria.
Amesema kuwa Mbunge huyo wamemkamata majira
ya mchana mjini Geita na kwamba wanaendelea na mahojiano ambayo yatasaidia kuwabaini wale ambao
walihusika na tukio.
Kamanda Mponjoli amesema jeshi lake
linaendelea na msako wa kuwabaini,kuwakamata na kuwachukulia hatua wale
wahusika wa tukio hilo na kwamba sheria
ya makosa ya jinai hayana kikomo na
kwamba mtu akifanya kosa leo na akakwepa
ataendelea kutafutwa,na hana namna ya kuukwepa Mkono wa sheria.
Mapema wiki
hii ,jeshi hilo lililazimika
kutumia nguvu kutawanya maandamano ya madiwani pamoja na wananchi walioweka
vizuizi katika barabara inayoingia mgodini wakishinikiza kulipwa ushuru wa
huduma kiasi cha dola za kimarekani milioni 12.65 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 26.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: