Baadhi ya wafanyabiashara (wajasiriamali) wadogo na wa kati walioshiriki mkutano ulioandaliwa na benki ya CRDB mkoani Mwanza kwa ajili ya kujadili pamoja masuala mbalimbali ya kibenki ili kusaidia kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Na Binagi Media Group
Benki ya
CRDB leo imekutana na wafanyabiashara wadogo na wa kati mkoani Mwanza na
kuwahakikishia kwamba itaendelea kutoa huduma bora ikiwemo mikopo ili kukuza
mitaji yao.
Akisoma
hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt.Charles Kimei, Mkurugenzi wa
CRDB tawi la Mwanza, Wambura
Calystus amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa
kwa wakati wote katika benki hiyo kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.
Amesema
benki hiyo imeendelea kutanua na kuboresha huduma zake ikiwemo uwepo wa Matawi
20, vituo vya kutolea huduma 50, ATM 135, mawakala wa Fahari huduma zaidi ya
649 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Aidha
amesema kwa mkoa wa Mwanza benki ya CRDB ina matawi manne, vituo vya huduma 13
pamoja na Mawakala wa Fahari Huduma zaidi ya 105 na hivyo kusaidia kuwafikia
wateja wake kwa urahisi.
Baadhi ya
wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Agapiti Malya pamoja na Doroth
Baltazari wameipongeza benki hiyo kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo
na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi
huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoani Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huu, hii leo Jijini Mwanza
Meneja Mwandamizi wa benki ya CRDB, kwa wateja wadogo na wa kati, Elibariki Masuka akizungumza kwenye mkutano huo Jijini Mwanza
Meneja Biashara benki ya CRDB, Danford Muyango akizungumza kwenye mkutano huo
Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada kwenye mkutano huo
Benki ya CRDB imeendelea kuwahakikishia wajasiriamali kwamba itaendelea kushirikiana nao kwa kuwapatia mikono yenye riba nafuu ili kukuza biashara zao
Mjasiriamali Doroth Baltazari ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Chabati Pop Food, akiwaonyesha baadhi ya wanahabari bidhaa anazotengeneza.
Attachments area
Preview YouTube video BENKI YA CRDB YAWAHAKIKISHIA WATEJA WAKE MIKOPO
Post A Comment: