WANASHERIA NCHINI KENYA WALAANI TUKIO LA KUPIGWA RISASI KWA TUNDU LISSU

Share it:
Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimelaani vikali  tukio la kupigwa risasi Rais wa Chama cha Wanasheria  wa Tanganyika (TLS),  Tundu Lissu.

Rais wa LSK, Isaac Okero amesema tukio hilo limewashtua  wanasheria wote wa Kenya.

“Tumepata taarifa kwamba Lissu amepigwa risasi akiwa kwenye gari lake mjini Dodoma, kwa kweli imetushtua sana na inahuzunisha,” amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

“Kwa pamoja tunalaani tukio hilo kwa kuwa hili limewagusa wanasheria wote wa Afrika na hata dunia kwa jumla.  Tunasikitika kwa uvunjifu wa sheria uliofanyika,’’ amesema.

Amesema Lissu anafahamika kwa kutetea haki za binadamu, hivyo wanasheria wote wapo pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake na Mungu atamsaidia atarudi katika hali yake ya kawaida.
 CHANZO MPEKUZI
Share it:

JOEL MADUKA

matukio

Post A Comment:

Also Read

BINTI WA MIAKA 16 ALAZIMISHWA KUOZWA NA BABA YAKE MZAZI BAADA YA KUSHINDA KUENDELEA NA KIDATO CHA KWANZA

Mtuhumiwa Bw,Saayai Petro ambaye anashitakiwa kwa kumuoa Binti wa miaka 16 akiwa amekamatwa. Mzee Kashirima Kashim

JOEL MADUKA