JAMII YAASWA KUENDELEA KUWASAIDIA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU MKOANI GEITA

Share it:
Watoto wa kituo cha kulelea watoto ambao wanatoka kwenye mazingira Magumu Mkoani Geita cha Brith Light wakiwa kwenye sherehe ya chakula cha mchana pamoja kuchangia mahitaji mbali mbali ambayo yanawakabili kituoni hapo.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mkoani Geita Robart Ngai akisisitiza watu kuendelea kuwa na moyo wa kujitolea kuwasaidia watoto ambao wanakabiliwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za kielimu pamoja na maradhi ili kujenga Taifa la kesho ambalo litakuwa na Elimu.

Watoto wa kituo cha Brith Light wakiimba wakati wa sherehee za chakula cha mchana.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa wakiendelea kufuatilia na kusikiliza kwa umakini kile ambacho kilikuwa kikiendelea meza Kuu.

Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto cha Brith light  Methiw Daniel akisisitiza jamii kuendelea kuwaona watoto ambao wanaishi mazingira Magumu kuwa ni mtoto wa kila mtu na kwamba wajibu wa kuwasaidia na wa kila mwanajamii.


Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino Mkoani Geita,Isaack Timothi amewahasa wananchi Mkoani Geita kuwa na mwitikio wa kuwasaidia watoto na kuachana na maswala ya ubinafisi.

Ayoub Ambaye anatoka taasisi ya marafiki wa Elimu akielezea mikakati ya kuendelea kushirikiana na taasisi Hiyo ambayo imejitolea kuwasaidia watoto wanatoka mazingira magumu.


Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ambaye alitarajia kuwa mgeni rasmi kwenye hafra ambaye ni  ,Afisa maendeleo ya Jamii halmashauri ya mji wa Geita ,Bi Mariam John akielezea  mikakati ya serikali kusaidia kituo hicho.

Makamu Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoani Geita Victor Bariety akikabidhi katoni za sabuni ambazo zimetolewa na chama hicho.

Watoto wa kituo cha kulelea watoto cha Brith Light wakisalimiana na Mgeni Rasmi pamoja na wagenu wengine ambao walikuwa meza Kuu.

Watoto pamoja na wageni waalikwa  na mgeni rasmi wakipiga picha ya pamoja.
PICHA NA JOEL MADUKA.




Jamii Mkoani Geita imeaswa kuendelea kujitolea na kuwasaidia watoto ambao wanatoka kwenye mazingira magumu na hatarishi.

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa makanisa ya EAGT mkoani Geita Mch Robart Ngai wakati wa dhima ya chakula cha  mchana na watoto wenye ualbino  na wale ambao wanatoka kwenye mazingira magumu .

Mch Ngai amesema kuna wajibu wa jamii kuwajibika na kuwasaidia watoto ambao wanaishi mazingira magumu ili kuweza kujenga Taifa lenye nguvu ambalo linakuwa na watu ambao wamepata elimu na kufanya hivyo ni kutimiza kusudi na agizo la Mungu.

Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto cha Brith light  Methiw Daniel ,amesema kuwa kila mtanzania na kila raia anajukumu la kumuhudumia mtoto pasipokujali kuwa wa kwake au sio wa kwake.

Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya  ,Afisa maendeleo ya Jamii,Bi Mariam John ,ameendelea kusisitiza kuwa ni wajibu wa jamii kushirikiana na taasisi ya Brith light kuweza kusaidia taasisi hiyo  kwa kupatiwa huduma za msingi za kila siku na kwamba mtoto sio mali ya serikali bali ni kila mtu anahusika kutoa msaada.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino Mkoani Geita,Isaack Timothi amewahasa wananchi Mkoani Geita kuwa na mwitikio wa kuwasaidia watoto na kuachana na maswala ya ubinafisi.

Share it:

habari

Post A Comment: