|
Naibu mkurugenzi toka mamlaka ya
mawasiliano Tanzania (TCRA)
Thadayo Ringo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina ya kuelekezwa namna ya kuhama mtandao bila ya kubadilisha namba ya simu. |
|
Mwandishi mwandamizi wa Nipashe na RFA Mkoani Geita Renatus Masuguriko akiuliza swali wakati wa semina. |
|
Mhandisi
mwandamizi Mwesigwa Felician kutoka TCRA akiendelea na semina kwa waandishi wa habari Mkoan Geita. |
|
Mhandisi Mwandamizi Mwesigwa Felician kutoka TCRA akitoa maelekezo kwa wanasemina ambao ni waandishi wa habari Mkoani Geita. |
|
Waandishi wa habari Mkoani Geita wakifuatilia semina kutoka TCRA. | | | |
|
PICHA NA JOEL MADUKA.
Wananchi Wilayani Geita wametakiwa kuwa makini pindi
wanapotumia mitandao ya simu hasa wakati wa huduma za miamala ili kuepusha
usumbufu utokeao kwa makosa ya miamala
hiyo kwa kuhakiki mara tatu kabla ya kutuma muamala huo.
Wito huo umetolewa na
naibu mkurugenzi toka mamlaka ya
mawasiliano Tanzania (TCRA)
Thadayo Ringo wakati wa semina kwa waandishi wa habari
mkoani Geita juu ya huduma ya
kuhama toka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila
kubadili namba ya simu na kusema
kuwa uhahikiki wa muamala kabla ya kutuma ni muhimu ili kuepuka changamoto za
malalamiko ya kupotelewa fedha.
Akizungumzia faida za
huduma ya kuhama toka mtandao mmoja wa
simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu kwa mteja, mhandisi mwandamizi Mwesigwa
Felicia kutoka TCRA amesema huduma hiyo
inampa nguvu mteja kuchuja huduma bora zaidi toka mtandao mmoja kwenda mwingine
pasipo kuhofika kubadilka kwa namba na kuongeza
ushindani kwenye sekta ya mawasiliano.
Post A Comment: