Mbunge wa jimbo la mafinga
mjini Cosato Chumi akitoa maelezo wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano
Mbunge
wa jimbo la mafinga
mjini Cosato Chumi akipeana mkono na viongozi wa timu ya Mafinga veterani wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa
timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi
cha shilingi laki Tano
Na fredy Mgunda, Mafinga
Mbunge wa jimbo la mafinga
mjini Cosato Chumi amezipiga tafu timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ngazi
ya mkoa wa Iringa kwa kuzipatia jozi moja moja ya jezi kwa kila timu lakini pia
ameichangia timu ya Mufindi United inayoshiriki lingi daraja la kwanza Tanzania
bara kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuisaidia katika harakati zake
za kupanda daraja.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi vifaa na pesa hizo Chumi alisema kuwa ameguswa kufanya hivyo kwa kuwa
anapenda michezo na anacheza mpira wa miguu kufanya hivyo kutaendelea kuzipa morali
timu za jimbo la Mafinga Mji kufanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki.
"Leo nimekabidhi jezi kwa
timu zinazoshiriki daraja la tatu ngazi ya mkoa na timu hizo ni Bajaji Fc,Mabo
Fc (Boda Boda) na Kinyanambo United nimefanya hivyo kuzifanya timu hizi
kuzihamasisha kufanya vizuri kwenye ligi hiyo" alisema Chumi
Chumi aliwataka wananchi na
wadau wanaoipenda timu ya Mufindi United kuendelea kuisaidia katika haraka za
kupanda daraja kwa kuwa kuendesha timu ni gharama kubwa hivyo tuungane kwa
pamoja kufanikisha lengo letu ili kupata timu itayokuwa ligi kuu Tanzania Bara
msimu ujao.
“Jamani kushiriki ligi
daraja la kwanza ni gharama sana na ligi ya mwaka huu ni ngumu hivyo tunahitaji
kuwa na pesa nyingi kufanikisha lengo letu la kuwa na timu ya ligi kuu wenzetu
wengine wamejipanga sana na wanapesa hivyo timu yetu ikiwa na njaa itatuwia
vigumu kuipandisha” alisema Chumi
Aidha Chumi hakusita kuwapongeza
viongozi wa timu ya Mufindi United pamoja na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri
William kwa kuendelea kuisadia timu kushiriki lingi hivyo kwa michango na
mawazo yao.
“Mimi nilijua mwaka huu
tunashushwa daraja maana hali ilikuwa ngumu wakati wa usajili lakini viongozi
hawa walipigana kufa na kupona wakahakikisha timu inasajili na inacheza ligi
hiyo” alisema Chumi
Post A Comment: