Na George Binagi-GB Pazzo
Mratibu wa Shirika
la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa majumbani WOTESAWA, Cecilia Nyangasi (pichani juu) amesema shirika hilo limejiwekea mikakati ya kuhakikisha kwamba hadi kufikia
mwaka 2020 kusiwepo na mtoto chini ya umri wa miaka 18 ambaye ameajiriwa
kufanya kazi za nyumbani.
Nyangasi
ameyasema hayo hii leo kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari Jijini Mwanza, yaliyolenga
kuwajengea uwezo wa kusaidia kufikisha elimu katika jamii ili kuondokana na
mazoea ya kuwaajiri watoto kufanya kazi za nyumbani na hivyo kuwakosefa fursa mbalimbali
ikiwemo kupata elimu.
Amesema hatua
hiyo itasaidia kuwanusuru watoto wafanyakazi wa majumbani na ukatili ikiwemo wa
kingono pamoja na kiuchumi ambapo baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi bila
malipo ama kwa malipo kidogo.
Aidha ametoa
rai kwa serikali kuboresha sera, mikakati na sheria zinazomlinda mtoto ili
kuondoa mkanganyiko uliopo ambao unashindwa kutambua bayana umri wa mtoto anayepaswa
kuajiriwa kwani baadhi hutaja umri wa miaka 14 huku nyingine ikitaja umri wa
miaka 18.
Nyangasi
amebainisha kwamba mwaka jana shirika la WoteSawa lilifanya utafiti katika Kata
nne za Jiji la Mwanza ambazo ni Igogo, Mkuyuni, Butimba na Capriont na kubaini
kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na utumikishwaji na
ili kupambana na hali hiyo shirika hilo lilianzisha mkakati wa kuwafikia watoto
waajiriwa, waajiri wao pamoja na viongozi wa serikali za mitaa na kuwaelimisha.
Nao
waandishi wa habari, Moses Mathew kutoka gazeti la Daily News pamoja na Rhoby
Magira kutoka Redio Afya wamebainisha kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuandika
habari na makala zinazoielimisha jamii ili kuondokana na mazoea ya kuwatumikisha
watoto kupitia ajira za majumbani.
Itakumbuka
kwamba mtoto mfanyakazi wa nyumbani analindwa na sheria kadhaa ikiwemo sheria
ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009, sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka
2004 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2017, waraka wa mishahara wa mwaka
2013 pamoja na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Kwa upande
wa waraka wa mishahara wa mwaka 2013, mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa
kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo
mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi
kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye
nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni ingwa
waraka huo hautaji mwajiriwa huyo anapaswa asiwe mtoto.
Mkufunzi Dotto Bulendu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostino cha Jijini Mwanza, akisisitiza wanahabari kuungana pamoja katika kuibua na kuandika habari/ makala zenye kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani
Afisa Habari shirika la WoteSawa akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mwanahabari Moses Mathew kutoka gazeti Daily News akichangia mada kwenye mafunzo hayo
Post A Comment: