Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu akiwaelezea wajumbe kuhusu swala la kuendelea kutimiza ilani ya chama cha mapinduzi(CCM). |
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wakifuatilia uchaguzi. |
Mbunge wa Jimbo la Busanda Lolesia Bukwimba akielezea mikakati ya kuendelea kupeleka maendeleo kwenye jimbo la Busanda. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita ambaye pia ni Mbunge Joseph Kasheku Msukuma akizungumza na wajumbe wa Mkutano huo. |
Wajumbe wakiendelea na kufuatilia Mkutano. |
Ukumbi ukiwa umesheheni wajumbe wa Mkutano huo. |
Msimamizi wa uchaguzi huo Joel Ramadhani Machanya ambae pia ni Katibu msaidizi na Mhasibu wa CCM Wilaya ya Mbongwe akitangaza matokeo ya uchaguzi. |
Kaimu Mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye alikuwa akisimamia uchaguzi Ahamed Mbaraka akikabidhi madaraka kwa mwenyekiti aliyechaguliwa. |
PICHA NA JOEL MADUKA.
Barnabas
Mhoja Mapande ,amechaguliwa kuwa
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Geita,kwa kupata kura754 na kuweka rekodi ya kukiongoza chama hicho
wilayani humo kwa awamu pili mfululizo .
Akitangaza
matokeo katika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa CCM wilayani humo ,msimamizi wa uchaguzi huo Joel Ramadhani
Machanya ambae pia ni Katibu msaidizi na
Mhasibu wa CCM Wilaya ya Mbongwe , amesema kura ambazi zilipigwa ni 1291 na
ambazo ziliharibika ni 166 hivyo kura harari 1125.
Amesema kuwa
,Mapande ameshinda dhidi ya
wagombea wenzake Alhaji Saidi Mganda
Mahoma alipata kura 35 na Adoado Ntwane Kazihoba amepata kura 336.
Aidha
Machanya ameendelea kutaja nafasi
za wajumbe watakaowakilisha mkutano
mkuu Taifa kutoka CCM wilaya, kuwa ni Leornad Kiganga Bugomola Kura 657 ,Herman
Clement Kapufi kura 681 na Constatine Molandi Mtani Kura 777.
Awali
mbunge wa jimbo la Geita Mjini
Constatine Kanyasu ,amesema kazi yake kubwa ni kuendelea kusimamia ilani ya chama kwa kuwatumikia wananchi
wa jimbo huku akielezea shughuli ambazo
hadi sasa ameendelea kuzitekeleza likiwemo swala la kupeleka umeme kwenye
maeneo ambayo yapo nje ya mji pamoja na kuboresha miundo mbinu ya Barabara kwa
kiwango cha Lami na Molamu na kwamba atahakikisha anashirikiana na viongozi hao
kujenga na kutengeneza misingi mipya ya CCM mpya ,ili kutimiza madhumuni na
kusudi la mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.
John Magufuli .
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mbunge Joseph Kasheku(Msukuma)ameewataka
madiwani wa halmashauri mbili ya mji na Wilaya ambao hivi karibuni waliandamana
kuelekea mgodi wa GGM wakishinikiza kulipwa madai ya kiasi cha sh Dola Milioni
12, ambao bado hawajafika polisi kwenda kwa pamoja kwaajili ya kusikiliza kile
ambacho wanatakiwa kwenda kukijibu huku akidai yupo tayari kuendelea kukamatwa
na Jeshi la Polisi kwasababu ya masirahi ya wananchi.
Kwa
upande wake Barnabas Mhoja Mapande
,amewashukuru wajumbe
waliomchagua na ambao awakumchagua na
kuwataka kuvunja makundi ili kuendelea
kukijenga chama hicho .
Alisema
kuwa wajibu wa chama hicho ni kusimamia
serikali na kwamba wajibu wa serikali ni kuendelea kuhimiza utekelezaji wa
ilani ya chama hicho na wajibu wa mtumishi wa serikali ni kujua chama kinataka
nini hivyo kama kuna mtendaji na mtumishi ambaye anakwenda kinyume na
utekelezaji wa majukumu ni vyema wakakaa nao na kushughulika nao.
Pia
amewataka wagombea ambao alikuwa akigombea nao kuvunja makundi kwani uchaguzi
umemalizika ni vyema wakaenda kufanya kazi ili kuakikisha wanakitetea chama
hicho kwenye Nyanja na nafasi mbali mbali.
Post A Comment: