Baadhi ya watendaji
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wadau wa
Mashirika Yasiyo ya kiserikali nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga( hayupo pichani) wakati wa
zoezi la kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali
nchini.
Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini WAMJW
Serikali kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imehitimisha zoezi
la uhakiki kwa Mashirika Masiyo ya Kiserikali nchini ulioanza Mwezi Agosti
mwaka 2017.
Akizungumza wakati wa
kutoa taarifa kwa umma kuhusu kukamilisha zoezi hilo Katibu Mkuu Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa jukumu la Wizara
ni kusajili na kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mujibu
wa Sera ya kitaifa ya Mashirikka Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001.
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha uratibu wa mashirika yasiyo ya
kiserikali nchini kwa kuimarisha mifumo ya uratibu kwa kushirikiana na
Halmashauri zote nchini.
Bibi Sihaba Nkinga
ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia Sheria, taratibu na
kanuni zilizopo katika kuendesha kazi zao katika kuhudumia jamii.
“Tumekamilisha zoezi
hili kwa kipindi tulichokiweka na ninawaomba wadau wetu wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali nchini kuzingatia Sheria na
taratibu zilizopo katika utendaji wa shughuli zao la kila siku” alisema Bibi
Sihaba.
bibi Sihaba mefafanua kuwa Mashirika
ambayo hayakuweza kuhakikiwa kwa sababu za msingi katika kipindi chote
cha uhakiki, yanatakiwa kufika Ofisi ya Msajili wa NGOs ili kukamilisha
zoezi hilo na mara baada ya tarehe hiyo muda wa uhakiki utasitishwa na
mashirika hayo hayataruhusiwa kufanya kazi yoyote nchini kwa kushindwa
kuzingatia taratibu.
Kwa upande wake Msajili
wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Marcel Katemba amewashukuru wadau
wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwa kujitokeza kuhakiki Mashirika yao
na kuwaomba kuendeleza ushirikiano uliopo kati yao na Serikali.
“ Niwashukuru wadau
wetu kwa kujitoa kwao na kuona umuhimu wa kushiriki na kuwa waangali wa zoezi
hili la uhakiki wa Mashirika yao” alisema Bw. Katemba.
Naye Katibu Mkuu wa
Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Ismail Suleiman ameishukuru
Serikali kwa kuendesha zoezi la uhakiki wa mashirikka hayo nchini kwa lengo la
kusaidia kukuza ufanisi wa kazi zao.
“Tunaishukuru
Serikali kwa zoezi hili ambalo litatusaidia kuendesha shughuli zetu kwa
kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo”alisema Bw. Suleiman.
Post A Comment: