Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe. Deogratius
Ndejembi akisisitiza jambo alipokutana na ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu
ulipotembelea Wilaya hiyo mapema leo ukiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA
wa Tume hiyo Bi. Devotha Gabriel.
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa
Walimu akimuonesha Katibu Msaidizi wa
Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Bw. Edward Chamwela namna ya kutumia mfumo rasmi wa
barua pepe za Serikali (GMS) ili kuimarisha Mawasiliano ngazi ya Wilaya na
Taifa.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO Dodoma)
Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) imetajwa kuwa kiungo muhimu
katika kuwawezesha walimu kutoa mchango wao utakaosaidia kukuza Kiwango cha
elimu hapa nchini.
Akizungumza wakati wa ziara ya Ujumbe wa Tume hiyo Wilayani
Kongwa Mkoani Dodoma Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa
anaipongeza Tume hiyo kwa kuweka mkazo katika matumizi ya TEHAMA.
“Teknolojia ni jambo muhimu sana katika kusaidia kuharakisha
maendeleo na kuongeza ufanisi kwa kuondoa udanganyifu unaoweza kujitokeza
katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuwahudumia wananchi “ Alisisitiza
Ndejembi
A
kifafanua zaidi Mhe. Ndejembi
amesema mifumo ya TEHAMA inayoenda sambamba na mahitaji ya ulimwengu wa sasa ni
chachu ya maendeleo hapa nchini.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Audiphace
Mushi amesema kuwa Tume imewezesha walimu kutambua haki na wajibu wao,kusaidia
walimu kupata haki zao kwa wakati.
Tume ya utumishi wa Walimu imekuwa mhimili muhimu katika
kuwasimamia walimu hivyo ni vyema kila mdau akasaidia juhudi za Tume ili
kuimarisha utendaji wake.
Tume ya Utumishi wa Walimu imetembelea Wilaya za Chemba,
Bahi, Chamwino,Kondoa, Mpwapwa na Kongwa ili kujionea hali halisi ya utendaji
wa Makatibu Wasaidizi wa Tume ngazi ya Wilaya hali itakayochochea na
kuhamasisha wadau kujitokeza na Kusaidia Tume kukabiliana na changamoto
zinazowakabili walimu kote nchini.
Post A Comment: