"SHULE ZENYE WANAFUNZI ZAIDI YA ELFU TATU ZINATAKIWA KUTAFUTIWA MAENEO YA KUJENGWA SHULE MPYA"PROF MSANJILA.

Share it:
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila  akizungumza na wanafunzi wa shule ya watoto wenye uhitaji maalum ya Mbugani iliyopo Wilayani na Mkoani Geita.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinaly Akizungumza na kuelezea hali ya elimu ilivyo Mkoani Geita.

Mwl Huruma Yusuf akielezea namna ambavyo wamekuwa wakiwafundisha wanafunzi ambao wanauhitaji na vifaa ambavyo wanafundishia wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof, Simon Msanjila alipokuwa akitembelea na kujionea vifaa hivyo vya kufundishia.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila  pamoja na Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa chuo kikuu huria tawi la Geita wakizungumza kwenye ofisi yake wakati alipotembela chuoni Hapo.


Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akiwatunza watoto ambao wanasoma kwenye shule ya watoto wenye uhitaji maalum wakati walipokuwa wakiimba.


Na Joel Maduka wa Maduka Online.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila amesema shule zenye wanafunzi zaidi ya elfu 3 ni vema zikatafutiwa maeneo na kujengwa shule nyingine ili kupunguza msongamano wa wanafunzi.

Amesema wakati wa ziara ya siku moja Wilayani Geita baada ya kupokea taarifa ya wilaya ya Mkuu wa Wilaya hiyo Bw Herman Kapufi kuhusu upungufu wa vyumba vya madarasa na msongamano wa wanafunzi kwenye shule za msingi wilayani humo.

Bw Kapufi amesema wilaya hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 755 hali ambayo imeendelea kusababisha mlundikano wa wanafunzi .

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu huyo Prof. Msanjila amesema tatizo hilo la upungufu wa vyumba vya madarasa na idadi kubwa ya wanafunzi linapaswa kutatuliwa kwa kujengwa shule mpya kwenye eneo tofauti na ilipo ya sasa.

Alipotembelea Shule ya ekndari ya Nyankumbu Wasichana, Prof Msanjila ameagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini sababu za shule hiyo kutowahi kufaulisha mwanafunzi wa daraja la kwanza.


Share it:

habari

Post A Comment: