Na,Consolata
Evarist ,Geita
Chama cha
mapinduzi(CCM)Wilaya ya Geita kimefunga
kampeni zake za kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Senga,huku kikiahidi
kuendelea kutekeleza na kutatua matatizo ya wananchi kwenye kata hiyo.
Akimnadi
mgombe udiwani wa kata hiyo,Mwenyekiti wa ccm Mkoani humo,ambaye pia ni mbunge
wa Jimbo la Geita,Joseph Msukuma,alisema kuwa chama hicho kimeendelea
kujidhatiti kwa kutatua kero
mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za
afya ,miundombinu ya barabara hususani zile za vijijini na umeme.
“Rais
Magufuli ametupa lami kilomita hamsini
na saba kutoka Geita kwenda Nkome bado
tu mnaendelea kuchagua upinzani inatakiwa tuwe kimya ili tujengewe bugando yetu ndugu zangu na niwaombe ndugu
zangu tutulie na chama chenu ambacho kinampango mzuri wa kuendeleza maendeleo
na sio kuwa na siasa zisizo kuwa na maana nyie wenyewe mnaona wanachama wao
wanaama”Alisema Msukuma.
Msukuma aliendelea kusema kuwa kwasasa wameshaanza
kupima ngunzo za umeme na kwamba wanatarajia vijiji vyote kufikia mwakani viwe
vimesambaziwa umeme kwenye Mkoa wa Geita.
Aidha Mbunge
wa Jimbo la Geita,Mjini Constatine Kanyasu,alisema kuwa kampeni za kutoa ahadi
ziliishia mwaka 2015 kwani kwasasa wanaye mbunge ,Rais na kwamba wao kama wananchi
wa kata ya Senga ni vyema basi wakahakikisha wanaunganisha nguvu kwa kumchangua
kiongozi ambaye anatoka ndani ya chama hicho.
Akiomba kura
kwa wananchi mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia (CCM),Thomas Tumbo,aliwaahidi
wananchi kushirikiana nao katika utatuzi
wa ujenzi wa zahanati,pamoja na vyumba vya madarasa ambavyo vimeonekana kuwa ni
changamoto kubwa kwenye kata hiyo.
Uchaguzi
mdogo wa kata hiyo unatarajia kufanyika jumapili ya Novemba 26 na vyama vinavyoshiriki ni
vitatu,CHADEMA,CUF na CCM.
|
Post A Comment: