NA COSTANTINE MATHIAS, BARIADI.
CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kimekabidhi mabati 74 yenye
thamani zaidi ya shilingi 900,000 kwa ajili ya kupaulia nyumba ya Mganga katika
zahanati ya Ikungulyandili.
Akikabidhi
msaada huo, Katibu wa CCM wilayani hapa Nicholaus Kasendamila alisema kuwa
wanatoa mchango huo ili kukamilisha ujenzi na pia kuunga mkono nguvu za
wananchi waliojenga boma la nyumba hiyo.
Kasendamila
aliwataka viongozi wa kijiji hicho kuyatumia ipasavyo mabati hayo kama
yalivyoelekezwa, huku akisisitiza juu ya usimamizi wa rasilimali za chama na za
serikali.
‘’baadhi ya
viongozi wa chama na serikali wamekuwa wakihujumu mali za chama kwa kuona kuwa
hazina msimamizi…lakini niwaombe kwa yeyote aliyehujumu mali ya chama
hatutasita kumchukulia hatua’’ alisema Kasendamila.
Akiongea
mara baada ya kupokea mabati hayo, Mtendaji wa kijiji hicho Magembe Charles
alimhakikishia katibu huyo kuwa baada ya siku tatu, watakuwa wamekamilisha
kupaua jengo hilo kwa sababu wameshapandisha kenchi na vifaa vingine vipo.
Katika hatua nyingine chama hicho kimepokea wanachama wawili ambao ni mwenyekiti wa kijiji cha Mwasilimbi-Ihusi na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwakitwala-Ihusi waliohama kutoka chadema kurudi CCM.
Wakiongea
mara baada ya kukabidhi kadi zao walisema kuwa awali walishawishiwa na baadhi
ya watu, lakini kwa sasa wamekuwa hawana msaada kwao wakiwafananisha Chadema na
mwindaji aliyeenda porini na kumwacha mbwa awinde bila kumsaidia.
‘’ nimeona
chama kimepoteza mwelekeo na hakipo…sawa na mtu aliyesindikiza mbwa kwenda
kuwinda halafu yeye akarudi kulala, nimeamua kuhama mwenyewe na wala
sijashinikizwa na mtu yeyote’’ alisema Ng’ombe Ntemi aliyekuwa Mwenyekiti wa
kijiji cha Mwasilimbi.
Post A Comment: