![]() |
Baadhi ya viongozi wa mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) Wakiwa na nyuso za furahaa wakati wa sherehe za usiku wa Mtanzania. |
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu
Geita(GGM) Bw Richard Jordinson (wa Pili kushoto)
akichukua chakula chenye asili ya Mtanzania.
|
![]() |
Mkurugenzi
Mtendaji wa GGM Bw Richard Jordinson (kulia) akimkabidhi Zawadi ya Picha,
Msanii wa Filamu Bi,Rosemery Michael baada
ya Kutangazwa Mshindi bora kwenye Vazi la Asili.
|
![]() |
Msanii wa Muziki wa Dansi Christian Bella(Katikati) akitumbuiza kwenyeTamasha la Usiku wa Mtanzania akiwa na Bendi yake.
|
![]() | ||
Mshereheshaji kwenyeTukio la Usiku wa Mtanzania Stevie Nyerere(kulia) akimtambulisha Msanii Christian Bella(kushoto). |
MgodiwaDhahabuGeita (GGM)
umeadhimishaTamasha la Usiku wa
Mtanzania Jumamosi Tarehe 11 Novemba kwenye Ukumbiwa Desire Park Mjini Geita.
Akizungumza wakat iwaTamasha
hilo linaloutambulisha utamaduni wa Mtanzania,Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodiwa Dhahabuwa
Geita Bw Richard Jordinson amesema kuwa Tamasha hilo limeandaliwa kwa ushirikiano
waGGM,JamiiyaWatuwa Geita, Wakandarasiwa Ndani,Watoa huduma na wadau mbalimbali
wanaofanya kazi na Kampuni ya GGM mjini Geita.
“Tamasha la
UsikuwaMtanzanialilianzishwarasmimwezi April mwaka 2002
likisherehekewa pamoja na Sikukuu ya Muungano likikutanisha wafanyakazi Watanzania wanaofanyakazi ndani ya Mgodi wa Dhahabu Geita,BaadayeTamasha hilo lilifanyiwa marekebisho na kuanza kuadhimishwa mwezi Oktoba hadi Novemba kila mwaka ili kumuenzi pia
Baba waTaifa la Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere aliyefariki Dunia Oktoba
14 mwaka 1999”alisema Bw Jordinson
Bw Jordinson alisema kuwa
GGM
inajivunia kufanya kazi ndani ya Tanzania,nchi iliyoasisiwa kwenye misingi mikubwa ya Amani,umoja naUshirikiano,hivyo tukio hilo nikumbukumbu muhimu ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania.
.
Akitangaza Washindi Mbalimbali walio valia vizuri mavazi yenye asili ya Kitanzania kwenyeTamasha hilo,Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi wa Dhahabu
Geita Bw Charles
Masubi alisema kuwa Tamasha hilo ni fursa pia ya kutambua utamaduni wa Mataifa mbalimbali yanayo fanya kazi ndani ya Mgodi wa Dhahabu
Geita(GGM)
“GGM ilianza rasmi shughuli zake mwaka
2000
ikiwa na mchanganyiko wa Wafanyakazi kutoka mataifa mbalimbali,Mkurugenzi Mkuu wetu kipindi hicho Hayati
Harry Michael alianzisha utaratibu mzuri wa kila taifa kuwa na siku yake ya kuenzi utamaduni wao.
Tamasha
la Usiku wa Mtanzania linatukutanisha pia na Jamii ya Watu wa Geita
na Mataifa mengine kujifunza utamaduni mzuri wa Taifa la Tanzania
vikiwemo vyakula vya asili,ngoma,burudani na maonyesho”alisemaBwMasubi.
Akitoa neno la
Shukrani,Meneja mwandamizi wa GGM anayeshughulikia masuala ya Jamii Bw Manace Ndoroma
alisema kuwa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) unatambua umuhimu mkubwa wa Jamii ya Watuw a
Geita ndiyo maana umelifanyaTamasha hilo katikati ya Jamii ya Geita
ilikutoa fursa pia ya wao kujivunia Utamaduni wa Mtanzania
“Hizi ni jitihada kubwa za kukuza ujirani mwema kati yetu na Jamii ya Watuwa Geita.GGM inafarijika sana kuandaaTamasha kubwa
la
Usiku wa Mtanzania na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya Watanzania waishio mkoani Geita”alisemaBw
Ndoroma.
Post A Comment: