Mbunge
wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe, amesema anajipanga kulifungulia kesi ya
kikatiba jeshi la polisi nchini kutokana na kushikilia simu yake.
Zitto
ameeleza kuwa simu yake inashikiliwa tangu Novemba 7 mwaka huu
alipokamatwa kwa tuhuma za kuvunja sheria ya takwimu na sheria ya
makosa ya mtandao.
“Walisema
watahitaji simu hiyo kwa siku mbili tu, nilikwenda polisi KAMATA siku
tatu baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. Nimerudi leo
tarehe 20, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo”, amesema
Zitto.
==>Aliyoyasema Zitto kupitia akaunti yake ya Facebook:
Ndugu,
Jamaa na Marafiki, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 7/11/2017 Jeshi la
Polisi walichukua Simu yangu kwa ajili ya uchunguzi wao kuhusu tuhuma
dhidi yangu kwa mujibu wa sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya
mtandao. Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku 2 tu.
Nilikwenda
polisi KAMATA siku 3 baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na
uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20/11/2017, Polisi wanasema bado
wanahitaji simu yangu hiyo.
1) Nawakumbusha kuwa msitumie simu ile 0767777797 kwani bado imeshikiliwa na Polisi
2)
Katiba ya Nchi yetu kifungu cha 16(1) na (2) imeweka msingi wa nguvu
sana haki ya FARAGHA kwa raia na kwamba hata sheria ikitaka haipaswi
kuingilia mawasiliano binafsi ya Raia.
Nina
mashaka kuwa Jeshi la Polisi linakaa na Simu yangu muda wote huu kwa
sababu za zaidi ya uchunguzi wao wa makosa wanayonituhumu nayo. Nimeamua
kuwaachia Simu mpaka hapo watakapotosheka lakini wajiandae na kesi ya
kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika na
matumizi mabaya ya sheria ya Mtandao ( cybercrime act ).

Post A Comment: