CHIRWA,AJIB KUIKOSA MBAO FC JUMAPILI UWANJA WA CCM KIRUMBA

Share it:



Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania bara klabu ya Yanga inatarajia kusafiri leo kuelekea Mkoani Mwanza kwa ajili ya Mechi wao dhidi ya wenyeji timu ya Mbao FC utakaopigwa Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Yanga wanasafiri bila ya nyota wao ambao ni Ibrahim Ajib mwenye kadi tatu za njano,Obrey Chirwa yupo kwao Zambia kutokana na matatizo ya Kifamilia na pia itawakosa Kelvin Yondani,Thabani Kamusoko,Donaldo Ngoma bado wanasumbuliwa na majeruhi.

Habari njema kwa wana Yanga ni kurejea kwa mshambuliaji wao hatari Amis Tambwe ambaye mechi 11 za mwanzo alishindwa kucheza kutokana na majeruhi hivyo uwepo wake utaimarisha safu ya Ushambuliaji na ikumbukwe Mechi ya FA dhidi ya Teha FC alifunga bao la pili ambalo liliwapeleka hatua ya 32 bora.

Mbao FC tangu wapande Ligi Kuu ya Vodacom hawajawahi kupoteza mechi dhidi ya Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba wamekutana mara mbili kwenye uwanja huo mechi ya Ligi Yanga alifungwa goli 1-0 na pia wakakutana kwenye nusu Fainali ya FA Yanga aliweza kupoteza tena .

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu na utakuwa na upinzani Mkubwa kwani wenyeji wanataka kuendeleza Uteja kwa kuwafunga Yanga huku nao wageni wanatamba kuvunja mwiko wa kufungwa na Mbao Fc.

Ligi Kuu ya itaendelea kesho Azam FC watakuwa wenyeji wa Stand United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku na Jumamosi kutakuwa na mechi tatu, Lipuli na Tanzania Prisons Uwanja wa Samora, Iringa kuanzia Saa 8:00 mchana, Mtibwa Sugar na Maji Maji Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Ndanda FC na Simba SC Uwanja wa 

Nangwanda Sijaona mjini Mtwara zote zikianza saa 10:00 jioni.
Jumapili, mabingwa watetezi, Yanga watakuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza saa 10:00 jioni na Njombe Mji FC wataikaribisha Singida United kuanzia saa 8:00 mchana Uwanja wa Saba Saba, Njombe. 

Mechi za kukamilisha mzunguko wa 12 zitachezwa mwaka mpya, Januari 1 Mbeya City wakiikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Mwadui wakiikaribisha Ruvu Shooting zote kuanzia saa 10:00 jioni. Baada ya mechi hizo, Ligi Kuu itasimama tena kupisha mechi za Kombe la Mapinduzi visiwani.

 Zanzibar na raundi ya tatu ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwakani kabla ya kuingia kwenye mzunguko wa 13 wa ligi kuanzia Januari 13 na 17, 2018.
Share it:

JOEL MADUKA

michezo

Post A Comment:

Also Read

MVUA ZAUA WATU 7 MKOANI GEITA

Baadhi ya makazi ya watu yakiwa yamejaa maji kwenye mitaa ya Mwatulelo Kata ya Buhalahala Mjini Geita kutokana na mvua

JOEL MADUKA