Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Kangi Lugola akitoa maelekezo kwa mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM)mbele ya wananchi ambao walikuwa wamekusanyika kumsikiliza. |
Wananchi wa Katoma wakimsikiliza Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Kangi Lugola wakati alipokuwa akitoa maagizo.
Na,Consolata Evarist,Geita
|
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Kangi Lugola ameutaka
mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) kuwalipa fidia wananchi ambao wapo ndani ya
mgodi huo ndani ya mwezi mmoja,huku akiwapiga faini ya milioni Kumi kutokana na
uharibifu wa mazingira.
Alisema
mgodi huo umeonekana kuwa nje ya kiwango
cha kipimo ambacho kinaonesha vumbi
linalotoka linaathari kwa wananchi na kwamba kutokana kosa hilo mgodi umeadhibiwa kulipa faini ya
shilingi Milioni kumi ili kuendelea kulinda afya za watanzania .
Kangi
ameendelea kusema kwamba serikali ya Rais Magufuli haipo tayari kuona watu wake wanafanyiwa majaribio kwa
kuwavunjwa sheria ambazo zimewekwa kwaajili ya kuendelea kuyatunza na
kuyahifadhi mazingira.
Kuhusu
suala la fidia Naibu waziri ameutaka mgodi wa GGM pamoja na serikali Mkoani
Geita kuhakikisha wananchi ambao wapo ndani ya mgodi wawe wamelipa fidia wale
ambao wanazunguka maeneo hayo na kuwataka wamalize tatizo la kimazingira.
Diwani
wa kata ya Kalangalala Sospeter Mahushi alisema wananchi wameendelea kukosa
amani na furaha na kwamba ni vyema sasa serikali ikatoa tamko kama waendeleze makazi yao au GGM iwafidie
waweze kupisha maeneo hayo kwani wamekuwa wakipata shida pindi milipuko
inapotokea hali ambayo imekuwa ikiwaradhimu wengi wao kukimbia makazi wakati wa
shughuli za ulipuaji wa miamba.
Bi
,Elizabert Charles ambaye ni mkazi wa
mtaa wa Katoma alitoa malalamiko na kudai amepata matatizo ya kiafya kutokana
na milipuko ambayo imekuwa ikifanywa na mgodi wa Geita (GGM )na kwamba hakutendewa haki ya kimatibabu na
ameathirika.
Post A Comment: