KILA KIJIJI KUFIKIWA NA MRADI WA REA AWAMU YA TATU

Share it:
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akisoma taarifa ya maendeleo mbele ya Waziri wa Nishati Dkt,Medard Kalemani  mbele ya kamati ya ulinzi na usalama.

Waziri wa Nishati Dkt,Medard Kalemani  akisisitiza jambo mbele ya kamati ya Ulinzi na usalama baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Nicas Mayala akizungumza na wananchi wa Kijiji Bulega wakati alipofika kukagua miundombinu ya usambazaji wa umeme wa  REA  awamu ya Tatu.

Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat ,Maganga akiteta jambo na Waziri wa Nishati Dk,Medard Kalemani .

Mbunge wa jimbo la Bukombe  Doto Biteko akiwasisitiza wananchi wa Kijiji cha Bulega kutumia fursa ya umeme kujinufaisha kwenye miradi mbali mbali.
Na,Joel Maduka,Geita

Waziri wa nishati,Dkt Medard Kalemani amewaakikishia wananchi wa  kata ya Bulega Wilayani Bukombe Mkoani Geita  kwamba kila kijiji kitahakikisha kinafikiwa na mradi wa umeme wa REA na kwamba watakapoanza kuweka mitambo kwenye vijiji hakuna nyumba ambayo itaweza kurukwa watahakikisha zote zinafikiwa na mradi huo.

Kalemani ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua uwekaji wa umeme wa REA awamu ya tatu ambao unatarajia kuchukua miaka miwili ili kukamilisha zoezi hilo kwa maeneo yote ya vijijini.

Waziri Dk Kalemani amesema katika awamu ya kwanza na ya pili ya Mradi wa REA wilaya ya Bukombe haikuwepo lakini kwa awamu ya tatu wamefaidika na Vijiji 70 vimeingizwa katika mpango na ifikapo januari 12 mwakani umeme utakua tayari umewaka.

kuwa kwa maeneo ya vijiji vya Bukombe mkandarasi amesha jiandaa kufikisha nguzo tarehe 15 mwezi January mwaka 2018.

Naye Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko amewataka wananchi  ambapo umeme utakuwa umefika kwenye vijiji vya kutumia fursa hiyo kujinufaisha ikiwemo kufungua miradi ambayo itakuwa inatumia nishati hiyo.

Huku akiwasisitiza  wananchi hao kuendelea kumuunga mkono Rais  Magufuli kutokana na shughuli ambazo anazifanya likiwemo suala la kuleta nidhamu kwenye taasisi mbali mbali za serikali.


Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

WANAUME 800 WAFANYIIWA TOHARA GEITA

Baadhi ya vijana waendesha Piki piki (Boda boda)Wakionesha mfano wa namna mwanaume anaweza kujikinga na maambukizi ya

JOEL MADUKA