Waandishi wa habari wakiwa kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Geita. |
Mkurugenzi wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) Bw; Ladislaus Matindi akielezea namna ambavyo tiketi za ndege zitakavyokuwa zinapatikana pamoja na safari zilizopo kwa sasa hivi ndani ya shirika hilo. |
Na,Joel Maduka,Geita
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amekutana na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) Bw; Ladislaus
Matindi na kukubaliana kufungua Wakala wa Shirika hilo Mkoani Geita.
Akizungumza
Ofisini kwake baada ya mazungumzo hayo Mhandisi Robert Gabriel amesema Mkoa wa
Geita upo kwenye maandalizi ya kufungua Ofisi za Wakala wa Shirika la ndege
Tanzania ili kurahisisha na kuwa na usafiri wa anga wa uhakika kwa wananchi wa
Geita na nje ya Geita.
Mhandisi
Robert Gabriel ameongeza kuwa uwepo wa Shirika la ndege katika Mkoa wa Geita ni
fursa kubwa ya kuutangaza Mkoa na rasilimali zake kwa kuwa kutakuwa na watu
wengi wanaoingia ndani ya mkoa kutoka maeneo mbalimbali wakiwa na fedha hivyo
biashara zitakua ikiwemo sekta ya Utalii kwasababu kutakuwa na usafiri wa
Uhakika.
''Mkoa
wetu umekaa kimkakati kuna nchi za jirani za Rwanda na Burundi tutapata abiria
kutoka huko ambao watakuja Geita wakafanya biashara na kufanya utalii,pia Mkoa
unataka kuanzisha mnada mkubwa wa madini ya dhahabu hivyo uwepo wa huduma za
ATCL utafungua mkoa huu kwa kiwango kikubwa''.Alisema Luhumbi
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la ndege Tanzania Ladislaus Matendi amesema kuwa shirika
hilo linawarahisishia wakazi wa Geita kutumia huduma za ATCL wasiwe na haja ya
kwenda Mwanza kupata Tiketi bali wazipate hapa hapa Geita hivyo watazungumza na
wafanyabiashara ili kuanzisha wakala. Amesema Mkoa wa Geita una fursa nyingi
sana zikiwemo uchimbaji wa madini, bidhaa za Kilimo zinapatikana kwa wingi
hivyo Geita inaangaliwa kipekee.Ameongeza kuwa Mkoa una vivutio vingi hivyo ni
wakati wa ATCL kushirikiana na Mkoa, Bodi ya Utalii na TANAPA kunadi vivutio
hivyo.
Post A Comment: