Shamba la Mahindi ambalo limekauka kutokana na hali ya ukame kwenye kijiji cha Nyan’homango Kata ya Ilemela kilichopo Wilayani Chato. |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyan’homango Bw,Lameck Kajile akielezea changamoto ambazo zimejitokeza kutokana na hali ya ukame kijiji hapo. |
Fundi mitambo akiweka vyombo vya musiki sawa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Kwenye Kijiji cha Nyan’homango. |
Wnanchi wa kijiji cha Nyan’homango Kata ya Ilemela wakiwa kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la chato. |
Mkuu wa Wilaya ya Chato,Shaaban Ntarambe akiwashukuru wananchi ambao walijitokeza kwenye mkutano wa mbunge wa Chato. |
Na,Joel Maduka,Chato
Wakati neema ya mvua ikiendelea Mkoani Geita,Baadhi ya maeneo
Wilayani Chato yamekubwa na ukame ambao umesababisha mazao ya wakulima kukaukia
mashambani.
Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na kijiji cha Nyan’homango Kata ya Ilemela
ambapo mahindi yamekaukia mashambani kutokana na hali ya kukosekana kwa mvua
kwa muda mrefu kwenye maeneo hayo .
Mkuu wa wilaya Shambani Ntarambe akizungumza na kutoa taarifa ya
Wilaya Hiyo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Chato Dkt,Medard Kalemani ,amesema kuwa
maeneo mengi yameathirika kutokana na ukame hata hivyo amewataka wakulima
kulima mazao mbadala na yanayositahimili ukame ikiwemo zao la Mtama ili
kuepukana na baa la njaa hapo baadae iwapo hali hiyo itaendelea.
Wakizungumza baadhi ya wananchi na wakulima wa Kijiji cha
Nyan’homango akiwemo afisa mtendaji wa kijiji hicho Malimi Mkano wameelezea
kuwa hali hiyo imewaathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na kwamba wengi wao
walikuwa wanategemea mahindi ambayo yamekaukia shambani kupata chakula na
kwamba awakujua kama hali ya hewa itaweza kubadilika.
Kwa upande wake Mbunge wa Chato Dk. Kalemani ameelezea kuwa
mazao hayajaharibika sana na kwamba mazao mengi bado yapo vizuri pamoja na
changamoto za hali ya hewa bado wanamatarajio ya kupata chakula kingi kwenye Wilaya
hiyo na kwamba ameendelea kusisitiza wakulima kulima mazao ambayo
yanasitahimili hali ya ukame.
Post A Comment: