SANAMU YA MESSI YASHAMBULIWA NA KUHARIBIWA NA WATU WASIYOJULIKANA.

Share it:
Sanamu la Mess Limeshambuliwa na Kuharibiwa na Watu Wasiojulikana


Sanamu ya mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Leonel Messi limeshambuliwa na kuharibiwa na watu wasiyo julikana nchini Argentina.


Sanamu la mchezaji huyo mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or limekutwa limeharibiwa kwa kuvunjwa huku kikisalia kiatu tu katika eneo hilo ambalo ni jiji la Buones Aires nchini Argentina.

Hii ni mara ya pili kushambuliwa kwa sanamu hilo lililojengwa katika eneo ambalo yapo mengine ya wanamichezo mbalimbali kama wa NBA na bingwa wa Olympic Manu Ginobili na legendari wa Hockey, Luciana, mwanzoni mwa mwaka huu lilifanyiwa marekebisho kufuatia kuaharibiwa.

Messi mwenye umri wa miaka 30,licha ya kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu michuano ya kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi na kuwa na jumla ya mabao 61 katika michezo 123 aliyoichezea Argentina, mashabiki wanashindwa kuona mchango wake ukilinganisha na akiwa Barcelona kutokana na kushindwa kuipatia kombe la Dunia.
Share it:

JOEL MADUKA

michezo

Post A Comment:

Also Read

MAHAKAMA YAIKEMEA JAMHURI KUSHINDWA KUMPELEKA SETHI MUHIMBILI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeukemea upande wa Jamhuri kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumpeleka  mshtakiw

JOEL MADUKA