Na,Joel Maduka,Geita
Wakazi wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita,wameiomba serikali
kutekeleza kwa haraka miradi ya maji iliyoahidiwa kwa muda mrefu kutokana na
watu wengi kupata shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji
Baadhi ya wananchi hao Bi Anastazia Mashauri ambaye ni mkazi wa
Kata ya Ilemela na Bahati Mashauri ambaye ni mkazi wa Kata ya Muungano
wameelezea kuwa pamoja na jitihada ambazo serikali imeendelea kuzifanya
kuwapatia maji lakini hali bado mbaya kwani wengi wao hawapati maji safi na
salama.
"Hali ya upatikanaji maji kijijini kwetu ni mbaya sana kwani tunakisima kimoja tu hali ambayo imekuwa ikisababisha wengi wetu kuelekea ziwani kutafuta maji na maji ambayo tunachota ya ziwani yanakuwa sio masafi ila inaturadhimu kuchota tu kutokana na shida ya maji tunyopata hapa kijijini kwetu tunaomba serikali itusaidia kiukweli tunapata shida sana"Alisema Bi Annastazia Mashauri.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw
Bathoromeo Manunga amesema wanatarajia kutekeleza Miradi mikubwa miwili ya maji
ambayo itawanufaisha Wakazi elfu 62 ambapo kwa sasa ni asilimia 42 ya wakazi
wanaopata maji na salama.
Ameongeza kuwa mradi mmoja kati ya hiyo unategemea kuchukua maji kutoka
ziwa Victoria ambao utasambaza maji katika maeneo mbalimbali Wilayani Chato.
Mbunge wa Jimbo hilo Dr Medard Kalemani amewaambia Wananchi wa
Ilemela, Nyamboge na Kanyama kuwa awali walileta mradi wa visima vya kina
kirefu lakini bahati mbaya Mkandarasi alipokuja ilikua kipindi cha ukame na
maji hayakutoka na January 7 2018 Mkandarasi anakuja kupima tena.
Post A Comment: