Ugumu wa
maisha katika baadhi ya familia Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita umetajwa kuwa
moja ya sababu za wanafunzi wa kike wa sekondari kurubuniwa na wanaume kwa
kuwapa fedha na hivyo kupata mimba za utotoni.
Takwimu za
mimba kwa wanafunzi wa kike kwa shule za sekondari na msingi wilayani humo
katika kipindi cha mwezi January hadi Disemba mwaka jana zilikuwa mimba 52 na
kati ya hizo wanafunzi wa Sekondari ni 37 na wa shule ya msingi ni 15 na kwamba
wote walipoteza sifa za kuendelea na masomo.
Mkuu wa
Wilaya hiyo Bw Hamim Gweyama amesema miongoni mwa mikakati 10 walionayo kwa
mwaka huu kupambana na tatizo la mimba mashuleni.
Hata hivyo
katika mimba hizo 52, hakuna kesi hata moja iliyohukumiwa hadi sasa lakini ziko
kwenye hatua tofauti, na kesi 45 ziko polisi na upelelezi bado unaendelea
kufanyika na 7 ziko mahakamani ambapo mkuu wa wilaya hiyo amesema wana mikakati
mingi ya kuwalinda watoto wa kike.
Mimba kwa
wanafunzi zimetajwa kuongoza katika shule ya Sekondari ya Msalala ambapo
mtandao huu umezungumza na Mkuu wa shule Bw ,David Mayega alisema kuanzia mwaka
2016 hadi 2017 katika shule hiyo kumekuwepo na mimba zaidi ya kumi na kitu na
sababu kubwa ni umbali ambao wanafunzi wa kike wamekuwa wakitembea kwaajili ya
kufuata Elimu.
Aisha Said
ni mwanafunzi wa shule hiyo alisema kuwa muda mwingine wamekuwa wakifika
nyumbani wanakuta hakuna chakula hali ambayo imekuwa ikipelekea walio wengi
kuingia kwenye vitendo vya ushawishi na kurubuniwa na tamaa ya vitu vidogo.
Hata hivyo wilaya ya Nyang’wale impokea Sh
Milioni 150 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ambapo tayari
vifaa vimeanza kununuliwa na wakandarasi wanatafutwa kwa ajili ya kuanza ujeni
huo.
Post A Comment: