Baadhi ya wajumbe na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoani na Wilaya ya Geita wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Robert Luhumbi wakati alipokuwa akisoma taarifa ya Mkoa. |
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Mhe..Charles Mwijage akisisitiza ujenzi wa haraka zaidi wakati alipotembelea eneo la magogo lililopo kwenye halmashauri ya Mji wa Geita.
|
Na,Joel Maduka,Geita.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.
Charles Mwijage Amesema lengo la Serikali ni kuhamasisha
ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Jumuishi ambao unawahusisha watu wengi kupitia
viwanda vidogo na vya kati,vitakavyotumia malighafi zitakozozalishwa hapa nchini
vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini, ukiwepo mkoa wa Geita ambao
umeonekana kufanya vizuri katika eneo hilo.
Waziri Mwijage ameyasema hayo alipozungumza na
wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Geita wakati wa
ziara yake Mkoani humo, ambapo amesisitiza juu ya Ujenzi wa Uchumi
wa Viwanda ulio imara, shindani na endelevu, utakayozingatia mambo muhimu
matatu ambayo ni soko, malighafi na teknolojia.
Sanjali na Hayo Waziri Mwijage
amemtaka mkuu wa mkoa kuhakikisha anasimamia vyema ujenzi wa ofisi
za SIDO pamoja ujenzi wa majengo ya kufundishia wajasiriamali ambayo
yanatarajia kujengwa Wilayani Chato ili kufikia mwezi wa nne ujenzi huo uwe
umekamilika .
Pia ameongezea kuwa ujenzi wa ofisi ambazo
zitajengwa kwenye eneo la magogo litakuwa na eneo la kuwafundishia
wajasiriamali mbinu mbali mbali za kuanzisha viwanda vidogo pamoja na namna ya
kusindika bidhaa ambazo wanatakiwa kuziingiza sokoni.
Akiwasilisha taarifa ya Mkoa ,Mkuu wa Mkao wa
Geita Mhandisi Robert Luhumbi, amesema ili kuandaa mazingira mazuri
yatakayowawezesha wawekezaji kuvutiwa na kuwekeza mkoani humo Mkoa
umetenga maeneo 384 yaliyopo katika Halmashauri sita yenye ukubwa wa jumla ya
ekari 1,012 kwa ajili ya viwanda na ramani za mipango miji zimeandaliwa .
Luhumbi ametaja mikakati ya mkoa huo kwenye sekta ya viwanda kuwa
ni Kuanzisha kiwanda cha kuchakata muhogo na kufungasha ambapo maghala
mawili ya kuhifadhi muhogo na sokomoja yamejengwa na
kukamilika kupitia Programu ya Uboreshaji wa miundombinu ya masoko uongezaji
thamani na huduma za kifedha vijijini pia Kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama
katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ambapo andiko limeandaliwa na
kuwasilishwa katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa ajili ya
kupata mwekezaji.
Ameongezea kuwa Mkoa unaendelea kufanya mazungumzo na wawekezaji
walioonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha sukari. Aidha, tarehe 02
Januari, 2018 Mkoa umekutana na uongozi wa Bodi ya Sukari Tanzania kwa lengo la
kuanzisha kiwanda cha sukari katika Wilaya ya Geita.
Ofisi hizo zinazotarajia kujengwa kwenye eneo la
Magogo kwenye halmashauri ya mji wa Geita na Wilaya ya Chato
zinatarajia kuwa na maabara ndogo kwa ajili ya uzalishaji,Chumba cha
baridi kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa kama maziwa na kadhalika na kutakua na
mabanda ya watakayotumia wajasiriamli kwa muda.
Post A Comment: