Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi wakati alipowasili kwenye ofisi za Mkoa huo. |
Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe ,akisalimiana na mbunge wa Jimbo la Busanda Lolesia Bukwimba wakati alipowasili kwenye ofisi za Mkoa wa Geita. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akielezea hali ilivyo ya upatikanaji wa maji wakati wa kikao na wadau wa sekta ya maji Mkoani humo. |
Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe,akizungumza na wadau wa sekta ya maji kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa wa Geita. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM)Mkoa wa Geita,alhaji Said Karidushi akiwasisitiza watumishi kusimamia kwa makini zaidi miradi ya maji iliyopo kwenye Mkoa huo. |
Waziri wa maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe akiwa kwenye mradi wa maji uliopo kwenye kata ya Kalangalala. |
Na,Joel Maduka ,Geita
Waziri wa
maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe ameeleza kusikitishwa na kitendo cha kutokamilika kwa miradi ya maji
ya Inchukimya Bulamabupina, Nchankolongo na Nyamtukuza licha ya serikali
kutenga fedha nyingi kugharamia miradi
hiyo.
Akizungumza
na wadau wa maji, Mkoani Geita katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa huo Bw Kamwelwe
amesema amesikitishwa na mradi wa wilaya ya Nyang'hwale ambao umegaramiwa Sh
Bilioni 15 ambao hadi sasa umeshindwa kukamilika licha ya mikataba zaidi ya
kumi na moja kusainiwa.
Amesema
lengo la serikali ni kuona kufikia mwaka 2020, Watanzania hususani wa vijijini
wamepata Asilimia 85 ya maji safi na salama.
“Mimi
nimepewa dhamana ya kuhakikisha watanzania wanapata maji safi na salama na
ifikapo mwaka 2020 vijijini wapate asilimia themanini na tano kwasababu
serikali yetu inatenga bajeti ya utekelezaji wa miradi hii”alisema Kamwelwe.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amemwambia Waziri kuwa mkoa huo una tatizo la
upatikanaji wa maji kwenye maeneo mengi licha ya kuzungukwa na chanzo kikubwa
cha maji ya ziwa viktoria.
Mbunge wa
Busanda Lolesia Bukwimba akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Mkoa huo, alisema anaamini
ziara ya Waziri wa maji na umwagiliaji itasaidia kutatua kero ya maji
inayowasumbua wananchi kwa muda mrefu kwenye mkoa huo .
Waziri wa
maji na umwagiliaji Bw Isack Kamwelwe yuko Mkoani Geita kwa ziara ya siku 4
yenge lengo la kukagua miradi ya maji
Post A Comment: