Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiagana na
wananchi wa Wilaya ya Maswa mara baada ya mkutano wa Hadhara uliofanyika Uwanja
wa Nguzo Nane mjini Maswa.
|
Na Stella Kalinga, Simiyu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi mkoani
Simiyu kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuunga mkono jitihada za
Serikali katika maendeleo ya Sekta ya Elimu.
Mhe.Makamu wa Rais ameyasema hayo
wakati akizungumza na Wananchi wa Wilaya
ya Maswa Mkoani Simiyu kwenye Mkutano wa
hadhara uliofanyika Uwanja wa Nguzo Nane wakati wa ziara yake mkoani humo.
Amesema
Serikali imeamua kutoa elimu bila malipo na kuwapunguzia wazazi mzigo wa
kulipia gharama za karo na michango mbalimbali ya uendeshaji wa shule lakini
suala la kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu wananchi wanapaswa kuunga
kuchangia ili kuunga mkono juhudi hizo.
“
Tunapeleka fedha katika shule zote za Msingi na Sekondari ili wanafunzi waweze
kusoma vizuri lakini kwenye suala la ujenzi wa matundu ya vyoo, madarasa, maabara
pamoja na kwamba Serikali ina wajibu wa kufanya hayo na ninyi wananchi mnao
wajibu wa kusaidia kufanya hayo” alisema Mhe. Makamu wa Rais.
Wakati
huo huo Mhe.Makamu wa Rais ameipongeza Wilaya ya Maswa kwa kuongeza ufaulu
kutoka asilimia 45 hadi asilimia 75 kwa mwaka 2017 na akakemea vikali tabia ya
wanaume wanaoua ndoto za watoto wa kike kwa kuwapa mimba , ambapo amesema jicho
la Serikali liko kwa watoto wa kike na itawachukulia hatua kali wote
watakaobainika kufanya hivyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt.Seif Shekalaghe amesema watoto wa kike
28 wameripotiwa kuwa na mimba katika kipindi cha mwezi Desemba 2017 hadi sasa
na Serikali ya Wilaya kupitia Operesheni tokomeza Mimba imefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa 15 na kati ya hao wawili wamehukumiwa miaka 30 jela kila mmoja.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Madini , Mhe.Stanslaus Nyogo amewashukuru viongozi wa Wilaya kuleta
mafanikio katika elimu ikiwa ni pamoja na ongezeko la ufaulu.
Katika
hatua nyingine Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia
Suluhu Hassan mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Upasuaji Hospitali ya
Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING
THEATER” amewataka Watumishi wa Afya kufanya kazi kwa bidii.
Aidha,
amesema Serikali itahakikisha inaboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na
ujenzi wa vituo vya Afya katika kila kata na kuboresha huduma za Afya ya Mama
na Mtoto ili kupunguza Vifo vya mama na mtoto.
Naye
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Josephat Kandege amesema Serikali
imekusudia kujenga vituo vya Afya 286 kufikia
mwisho mwa mwaka 2017/2018 lengo
likiwa ni kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kupunguza mrundikano wa
wagonjwa katika Hospitali za Wilaya.
Mbunge
wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mhe.Mashimba Ndaki amesema pamoja na kuendelea
kuboresha sekta ya Afya kwa kujenga miundombinu, ni vema Serikali ikaajiri
watumishi wa Idara ya Afya kukabiliana na upungufu uliopo.
Mhe.Makamu
wa Rais amemaliza Ziara yake Wilayani Maswa ambapo amefungua Jengo la Upasuaji
la Upasuaji Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA
SULUHU HASSAN OPERATING THEATER” na kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa
Nguzo Nane.
Post A Comment: