|
Kutoka kushoto (wanaoandika) Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakisaini hati ya
makubaliano ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Nkoma
wilayani Itilima, fedha ambazo zimetolewa na Balozi wa China hapa nchini,
Mhe.Wang Ke., zoezi ambalo lilishuhudiwa pia na Makamu wa Rais wa Tanzania,
Mhe.Samia Suluhu Hassan Jana Mjini Bariadi.
|
|
Mwakilishi wa Shirika laUingereza la (
DFID) Bi. Elizabeth Arthy
akiwasilisha taarifa ya namna Shirika hilo linavyofanya kazi na mkoa wa Simiyu
mbele ya viongozi wa Kitaifa na Mkoa wa Simiyu, katika hafla iliyofanyika jana Viwanja
vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
|
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Itilima(mwenye miwani) na Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Wang Ke
wakisaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya
Sekondari Nkoma wilayani Itilima, fedha ambazo zimetolewa na Balozi huyo ,
zoezi ambalo lilishuhudiwa pia na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu
Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na viongozi wengine wa
Kitaifa na Mkoa mjini Bariadi.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akimshukuru Balozi wa China hapa Nchini, Mhe.Wang Ke
mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya
ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Nkoma wilayani Itilima,
fedha ambazo zimetolewa na Balozi huyo , zoezi ambalo lilishuhudiwa pia na
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan(katikati) na viongozi
wengine wa Kitaifa mjini Bariadi.
|
|
Balozi
wa China hapa Nchini, Mhe.Wang Ke akimkabidhi Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu
Hassan Hundi ya Shilingi milioni 178 kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la Wasichana
katika Shule ya Sekondari Nkoma wilayani Itilima, fedha ambazo zimetolewa na
Balozi huyo |
|
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akionesha Hundi
ya Shilingi milioni 178 iliyotolewa na Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Wang Ke
kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Nkoma
wilayani Itilima zoezi lililofanyika jana Mjini Bariadi.
|
|
Balozi
wa China hapa nchini, Mhe.Wang Ke akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu
Hassan(wa pili kulia) kabla ya kumkabidhi vyerehani 50 kwa ajili ya kikundi cha
wanawake Mjini Bariadi zoezi lililofanyika jana Mjini Bariadi |
|
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakati wa makabidhiano ya hundi ya ujenzi wa Bweni
Itilima, Vyerehani 50 viliyotolewa na Balozi wa China hapa nchini Mhe.Wang Ke
kwa kikundi cha wanawake Bariadi Mjini
na uwasilishwaji wa taarifa za mashirika wadau wa maendeleo mkoa wa Simiyu jana
jioni.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Shirika la
Mendeleo la Uingereza (DFID) kupitia Mpango wa Kuboresha Elimu
Tanzania(EQUIP-T) limetoa jumla ya shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya Elimu
katika Halmashauri zote za mkoa wa Simiyu.
|
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka wakati wa hafla fupi ya makabidhiano na
vyerehani 50 kutoka Ubalozi wa China, kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa
Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Nkoma Itilima, Makabidhiano ya. Hundi ya
Shilingi Milioni 178 kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo zilizotolewa na Balozi
wa China, na uwasilishwaji wa Taarifa za mashirika wadau wa Maendeleo mkoani
Simiyu(DFID, AMREF na UNFPA), ambayo ilishuhudiwa na Makamu wa Rais wa
Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Mtaka amesema
fedha hizo zimeshapokelewa katika Akaunti za Halmashauri zote za Mkoa huo na
wiki ya kuanzia tarehe 26/02/2018 Halmashauri hizo zinaanza kujenga miundombinu
ya Elimu.
Mtaka ametoa
shukrani zake kwa Shirika hilo ambalo amesema limechangia kwa kiasi kikubwa
mabadiliko katika Elimu na kuufanya mkoa wa Simiyu kutoka kwenye nafasi za
mwisho kwenye ufaulu mpaka kufikia nafasi ya 11 kwa mwaka 2017.
“ Tunawashukuru
sana DFID kwa namna wanavyotusaidia katika Sekta ya Elimu kwenye mkoa wetu, DFID kupitia EQUIP wametoa IPAD(Vishikwambi)
kwa kila Mkuu wa Shule ndani ya mkoa Simiyu, Kila Mratibu wa Elimu wa Elimu
Kata amepewa pikipiki na anapewa posho
ya shilingi 206,000/= kila mwezi kwa
ajili ya kununua mafuta ya kuwawezesha kutembelea shule zao,
sisi kama mkoa tunawashukuru sana” alisema Mtaka.
Akitoa taarifa
ya utendaji kazi wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) Bi. Elizabeth
Arthy amesema Shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na kuhakikisha wanashiriki katika kuinua
ubora wa elimu kwa watoto wa Mkoa wa Simiyu.
Naye Balozi wa
China hapa nchini Mhe. Wang Ke aliyekabidhi vyerehani 50 kwa ajili ya Kikundi
cha Wanawake Mjini Bariadi amempongeza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa jinsi anavyojishughulisha katika
kuwaletea wananchi wa Mkoa wa Simiyu maendeleo na akaahidi kuendelea
kushirikiana na mkoa huo katika nyanja mbalimbali.
Kwa upande wake
Mwakilishi Mkazi wa Shirika lilaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA), Bi.
Jacqueline Mahon amewapongeza viongozi wa mkoa wa Simiyu wakiongozwa na Mkuu wa
Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na akaahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za
maendeleo mkoani humo kupitia huduma za afya ya uzazi kwa wananwake na vijana.
Akitoa shukrani
kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhe.Andrew Chenge,
aliyashukuru mashirika hayo na Balozi wa China ambao ni wadau wakubwa wa
maendeleo mkoani humo katika Sekta ya elimu, afya na viwanda na kubainisha kuwa
mkoa huo una kiu ya maendeleo ni hivyo umejipanga kwenda kwa kukimbia wakati
wengine wanatembea.
Post A Comment: