Hospitali ya
rufaa Mkoani Geita inayojengwa Mtaa wa Magogo kata ya Bombambili mjini Geita
inatarajiwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya elfu moja wa nje na zaidi ya 480
watakaokuwa wakilazwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari walioambatana na Mwenyekiti wa bodi teule ya hospitali
hiyo, Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Glads Jefta alisema
katika hatua ya kwanza ya ujenzi wanaendelea na ujenzi wa majengo manne na
wanatarajia kukamilisha baada ya miezi 9 ambapo umefikia asilimia 35.
“Tunatarajia hospitali hii itakapokamilika itahudumia
idadi ya wagonjwa wa nje zaidia ya elfu moja na wa kulazwa mia nne na themanini
na tunaamini ndani ya muda wa miezi mitatu ambayo tumeomba kuongezewa tutakuwa tumekamilisha ujenzI”Alisema
Mhandisi Glads.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu alisema
matarajio walitarajia Hospitali hiyo ingekamilika ndani ya miezi 9 lakini
kukosekana kwa umeme na maji ndio sababu zilizokwamisha mradi huo kwa kuwa
Mkandarasi amekuwa akinunua maji kutoka nje na wakati mwingine kutumia mafuta
kwa ajili ya jenereta.
Kaimu mganga
mkuu wa Mkoa wa Geita Dr Joseph Odero alisema hospitali ya rufaa ya sasa ambayo
ilikuwa ya wilaya ni ndogo kwa kuwa ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 150 hadi 200 na wale wa kulazwa 200 hadi 250
na kwamba hali ya wagonjwa kwa sasa ni
kuanzia 300 hadi 350 hivyo kukamilika kwa hospitali hiyo ya rufaa kutasaidia
kukabiliana na changamoto ya wingi wa wagonjwa
Mradi wa
ujenzi wa hospitali ya rufaa kwa sasa
umefikia asilimia 35 kwa hatua ya kwanza ambayo inatarajia kugharimu kiasi cha
Sh Bilioni 5.9
Post A Comment: