Naibu waziri wa
madini Stanslaus Nyongo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano haiko
tayari kuona mtu akilalamika
,kunyanyaswa au kunyimwa haki yake.
kauli hiyo ameitoa wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Nyakabale
kata ya Mgusu Wilayani Geita
wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani humo ya kuzungukia maeneo ya
uchimbaji pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambao wanazunguka kwenye baadhi
ya maeneo ya mgodi wa Geita(GGM).
Hatua hiyo ya Naibu
waziri Nyongo imekuja baada ya kusikia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu
ya mgodi wa GGM kushindwa kuwalipa fidia kwa muda mrefu pamoja na kuwepo kwa
maagizo mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya viongozi ambao wamekuwa
wakifika Mkoani Humo.
Naibu waziri huyo alisema kuwa mtu mwingine yuko tayari kuona
Mtanzania mwenzake akikandamizwa ilimradi yeye
aendelee kulinda masilahi yake binafsi, na kwamba miaka
hiyo imeshapita muda uliopo kwa sasa ni kufanya kazi za kuwatumikia wananchi
ambao ni wanyonge.
“Tukikaa kwenye viyoyozi
hatuambiwi ukweli na wamiliki wa migodi lakini tunapo fika katika eneo husika
tunapata ukweli , unakuta mtu kazaliwa hapo kakulia hapo amejenga ana watoto
harafu mtu anakuondoa kwa madai kuwa upo kwenye leseni yake ainiingi akilini kama unahitaji eneo langu
njoo tukae tumalizane unipe changu mimi
nisepe inakuwa nilipe nisepe ”alisema Nyongo.
Hata hivyo aliwataka watu wa mgodi huo kuwalipa wananchi hao ama
waondoke wawaachie wananchi hao eneo lao waendelee kuchimba na sio kuwazuia
ikiwa hawafanyi shughuli za uchimbaji kwa sasa au wawaache waendelee kufanya
shughuli za bila kubuguziwa, mgodi ulikuja kama neema hivyo isiwe
mgodi huu kazi yake kuwanyanyasa wananchi.
Awali Akitoa malalamiko kwa Naibu waziri mwananchi wa Nyakabale kwa niaba ya wenzake Joseph
Kihengu alimwambia Naibu waziri kuwa wanailaumu
serikali iliyopita inawezekana wakati wanabinafsisha mgodi huu na
wao waribinafisishwa humo bila kujua.
“Mheshimiwa kipindi cha nyuma usingeweza kupata umati kama
huu, umati huu umetokana na imani ya serikali ya awamu ya tano waliyo nayo
hivyo serikali iwaangalie kwa jicho la tatu ili watu wanyakabele wajue hatima ya maeneo ambayo yapo ndani ya
bikoni mgodi wa GGM”Alisema Joseph.
Katika hatua nyingine akina mama wa nyakabale wakiwakilishwa na
Godliva Mgini waliutupia lawama mgodi huo wa GGM kwa kuwafilisi kwa kukilaghai
kikundi chao cha Baraka baada ya kuwaahidi kuwawezesha
kuanzisha mradi ufungaji wa nguruwe 100 ambapo waliambiwa
wasombe mawe ili wajenge na kujikuta wakighalamia kiasi cha shilingi laki nane baadae
wakatokomea kusiko julikana na kuwaacha maskini zaidi.
Nae makamu wa rais GGM Saimon Shayo alisema “tunatambua
majirani hivyo niseme tu baadhi ya maneno yaliyoelezwa hapa mengine yanafahamika
mengine ni mageni ndo tunayasikia na mangine tunahitaji kama
mgodi kukaa na kuyapatia ufumbuzi”.
Aidha alisema kuwa kuna baadhi ya watu wa nyakabale vigingi vyao
vipo ndani ya mgodi ambapo kimsingi jambo ili lipo wazi
pia kuna watu wana haki ya ardhi kisheria suala na kwamba suala hilo ni namna ya kukaa pamoja na kujadili kwasasa.
Post A Comment: