Naibu waziri wa madini Staslaus Nyongo Akizungumza na mmoja wa wamiliki wa mgodi huo Bw
,Alex Kindersley.
Na,Joel Maduka,Geita
Naibu Waziri
wa madini Stanslaus Nyongo amewataka wamiliki wa mgodi wa Nyarugusu Mine Company kuwalipa fidia haraka
iwezekanavyo wananchi 133 ambao
wapo kwenye kijiji cha Ziwani kata ya Nyarugusu Wilayani Geita kutokana na
kuharibiwa mazao yao na sumu ambayo ilitoka kwenye Bwawa la maji yenye sumu.
Agizo hilo
ambalo amelitoa Naibu waziri wa madini Nyongo limetokana na Wananchi hao ambao
wanadai kulipwa fidia ya kiasi cha sh,milioni 202 kufunga barabara ya mgodi huo
tangu Februari 18,mwaka huu kufuatia Mgodi huo kutoa majibu yenye utata.
Bi, Pili
Ramadhani alisema walipatwa na majanga hayo novemba
30 mwaka jana baada ya mazao yao kuharibiwa,na kwamba wamekuwa wanakabiliwa na njaa,hali ambayo
imesababisha kuhamua kuandamana huku wakikaa takribani wiki nzima kwenye maeneo
ya nje ya mgodi huo wakiitaji walipwe madai yao.
Mzee Slvanus
Matanywa (88) mkazi wa kijiji cha ziwani amejikuta akiangua kilio mbele ya
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akililia fidia yake kutokana na
kukabiliwa na njaa kwa kukosa chakula baada ya mazao yake kuharibiwa na sumu
hiyo.
“Nalia kwasababu wajukuu wangu awasomi
kutokana na kulala na njaa kwanini imekuwa namna hiyo sasa sijui nifanyeje sina chochote cha kunisaidia
watoto wakianza kulia nashindwa nifanye nini wewe ndiyo Baba maana tumeambiwa
tuheshimu mamlaka iliyo juu”Alisema Mzee Matanywa.
Nae
Mwenyekiti Wa Kijiji hicho Athuman
Seleman alisema ni kweli wananchi wake
tangu November mwaka jana mashamba yao
yaliingiliwa na matope yenye sumu na serikali imeendelea na jitihada za awali za
kufanya mazungumzo na mgodi ili walipe fidia shida ilikuja baada ya wamiliki wa mgodi kuleta barua ya kusema
hawawezi kutoa fidia kwa sasa mpaka wajiridhishe kutokana na vipengele fulani
hapo ndio lililipokuja tatizo.
“Shida iliyokuja ni kutokana na mgodi kugoma
kutoa fidia kwa madai wanataka baadhi ya vipengere wajiridhishe suala hili
limewakwanza wananchi na kweli kabisa mheshimiwa watu awa wanashida sanaa na
maisha yao yote walikuwa wanategemea mazao ambayo yanapatikana kwenye mashamba yao na maamuzi ya kufunga
mgodi yamekuja ni baada ya kukasirishwa na majibu ya mgodi”Alisema Mwenyekliti.
Kufuatia
malalamiko hayo waziri wa Madini Mh.Stanslaus Nyongo ameunga mkono hatua
iliyochukuliwa na wananchi wa Kijiji hicho kwa kufunga barabara inayoingia
kwenye Mgodi kutokana na kuwepo kwa majibu ambayo yamekuwa yakitolewa
ya kukatisha tamaa.
‘’ Naomba istafsiliwe
mlichokifanya ni makosa kufunga au kuzuia njia hii ya kuingia mgodini
mmefanya sawa sawa kwa sababu mnadai
haki yenu, nilikuwa namtafuta uyu mzungu toka jana lakini ninataarifa polisi
wamemkamata tayari’’ Alisema Nyongo.
Akizungumza
na mmoja wa wamiliki wa mgodi Bw ,Alex Kindersley Naibu waziri Nyongo amewataka kwa kushilikiana na mkuu wa
wilaya ya Geita kumaliza tatizo hilo ndani
ya wiki moja kulipa madai ya wananchi hao tofauti na hivyo kama wizara
watachukua hatua za kinidhamu dhidi ya
mgodi .
|
Post A Comment: