Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kufariki kwa mtoto wakati alipokuwa akiombewa.
Na,Joel Maduka,GEITA
|
Mtoto wa
miaka sita (6) ambaye anajulikana kwa jina la Frank Bariki amefariki wakati
alipokuwa akiombewa mlimani alikopelekwa kwaajili ya kutolewa mapepo kwa madai
alikuwa na taswira ya Bibi yake,huku mama mzazi
akishikiliwa na jeshi la polisi kwaajili ya upelelezi.
Kamanda wa
Polisi mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo alisema Tukio hilo lilitokea february 18,2018
majira ya saa tano asubuhi katika mlima wa Gambiwe kwenye kijiji cha Bukuru Wilaya ya Nyang’hwale.
Aidha amewataja wanawake hao kuwa Bi,Neema Petro(25) ambaye ni mama wa mtoto huyo na mke mwenzake Raheli Mussa (25) ambao wameolewa na Bw,Bariki Lunyaru walikuwa
kwenye kipindi cha mfungo wakiwa kwenye maombi yao wakati wakimuombea kwaajili
ya kumtoa mapepo ndipo walianza kumkamia mtoto huyo wakimshika na kumkaba
kwenye mbavu na kwenye shingo hali ambayo ilipelekea mtoto huyo kupoteza
maisha.
Kamanda Mponjoli ameendelea kusema wamechunguza mwili
wa mtoto wamebaini kulikuwa na alama za mikwaruzo kwenye maeneo ya shingoni na kwenye mashavu .
Ameendelea kufafanua kuwa hadi sasa bado hawajajua kiini cha tukio hilo ambalo limesababisha mtoto huyo
kupoteza uhai wakati alipokuwa akifanyiwa maombi ingawa hadi sasa jambo ambalo
wamebaini kuna viashiria vya vitendo vya
ushirikina ndani ya familia kutokana na madai ya taswira ya bibi yake .
Kamanda
Mponjoli alisema hadi sasa
wanawashikilia wanawake hao ambao ni wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang’hwale
kutokana na kifo cha mtoto huyo.
Post A Comment: