WAZIRI MWIGULU:GEREZA JIPYA CHATO KUPUNGUZA MSONGAMANO MAGEREZANI NA GHARAMA ZA USAFIRISHAJI WA WAHARIFU

Share it:
Mkuu wa Mkoa wa Geita(Kushoto)Mhandisi Robert Luhumbi na waziri wa mambo ya ndani(Kulia)Dkt,Mwigulu Nchemba (Katikati)Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa wakikata upete kwenye jiwa la Msingi wakati wa uzinduzi wa magereza Wilaya ya Chato.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu mkuu wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi wakati alipowasili kwenye viwanja vya hafla fupi ya uzinduzi wa magareza Wilaya ya Chato Mkao wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimpokea na kumsalimia waziri wa mambo ya ndani,Dkt Mwigulu Nchemba wakati alipowasili kwenye viwanja vya magereza wilaya ya Chato.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Nehemia Nkondo ,akisoma taarifa ya ujenzi wa magereza ya wilaya ya Chato.

Mkuu wa wilaya ya Chato,Shaaban Ntarambe akielezea manufaa ambayo yatapatikana kwenye wilaya hiyo kutokana na kufunguliwa kwa magereza.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amelitaka jeshi la magereza kupitia gereza la Wilaya ya Chato ambalo limejengwa kijiji cha Nyangomango kutumia maeneo yaliyopo na watakayopewa na Mkoa kuzalisha mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo. 

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa  akielezea madhumuni na dira ya magereza katika kutoa huduma kwa waharifu.

Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt.Mwigulu  Nchemba akizungumza na wananchi na baadhi ya askari ambao walikuwepo kwenye shughuli ya uzinduzi wa Gereza jipya wilaya ya Chato. 
Baadhi ya wakuu wa magereza pamoja na wananchi wakimsikiliza mgeni Rasimi ambaye ni Waziri wa mambo ya ndani,Dkt Mwigulu Nchemba alipokuwa akizungumza.

Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi na Waziri wa mambo ya ndani,Dkt Mwigulu Nchemba wakiteta jambo wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa gereza la wilaya ya Chato.

Waziri wa mambo ya ndani,Dkt Mwigulu Nchemba akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel  wakitoka kuweka jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa gereza la wilaya ya Chato.

Maafisa wa Jeshi la magereza wakiwa kwenye picha ya pamoja na waziri wa mambo ya ndani ,Dkt Mwigulu Nchemba pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita.

Na,Joel Maduka,Geita



Uzinduzi wa gereza jipya la Wilaya ya Chato  unatarajia kupunguza gharama za usafirishaji na msongamano wa wahalifu katika magereza mengine ambayo yalikuwa yakihifadhi waalifu kutoka Wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua wa Gereza  hilo , Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt.Mwigulu  Nchemba alisema katika Wilaya ya Chato kumekuwa na changamoto ya kutokuwa na Gereza na kulazimika kupeleka waarifu katika Gereza la Biharamulo hivyo gereza hilo litapunguza gharama za usafirishaji wa waharifu ambao wa walikuwa wakipelekwa magereza ya mbali ili kuhifadhiwa.

“ Ujenzi wa Gereza hili utasaidia kuendeshwa kwa mashitaka kwa kufuata ratiba kwa kuwa wakati mwingine ratiba zinaingiliana lakini pia changamoto za magari, mafuta na umbali zilikuwa kikwazo kikubwa katika uendeshaji wa mashitaka hivyo kusababisha watu wenye matatizo mbalimbali kuendelea kushikiliwa katika magereza kwa muda mrefu huku akikosa haki zake hata kama hana hatia”Alisema Mwigulu.

Aidha, Dkt Mwigulu nchemba ametoa rai kwa maafisa na askari wa gereza kuhakikisha wanatunza majengo na miundombinu ya gereza hilo na kufanya kazi kwa uadilifu ili maadili yaliyowekwa katika magerezani yanazingatiwa .

'' licha ya kazi nzuri inayofanywa na viongozi walio wengii zipo taarifa kwenye baadhi ya magereza watumishi hawazingatii maadili ya kazi kwa kuwa wengine wamekuwa wakiwapa waalifu simu bila kujua wanafanya mawasiliano na watu wa namna gani vitendo hivi vina hatarisha usalama wa gereza na askari pia''Alisisitiza Mwigulu.

Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amelitaka jeshi la magereza kupitia gereza la Wilaya ya Chato ambalo limejengwa kijiji cha Nyangomango kutumia maeneo yaliyopo na watakayopewa na Mkoa kuzalisha mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Mkoa na taifa.Ameongeza kuwa jeshi la magereza limejijengea heshima kubwa nchini kwa kuzalisha vifaa bora kama vile samani za nyumbani na ofisini, viatu hivyo jeshi linaweza kuleta mapinduzi ya kimkakati ya kiuchumi.


Naye Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Nehemia Nkondo ameeleza katika taarifa kuwa ujenzi wa Gereza la Chato ulianza mwaka 2011 katika kijiji cha Nyangomango kwa kupata hekari 50 kutoka kwa wananchi ambapo serikali ilitoa zaidi ya Shilingi bilioni 1.5 mpaka sasa mradi umetumia kiasi cha shilingi milioni 613.6 sawa na asilimia 40%. kiasi cha Shilingi milioni 903.6 zinaendelea kutumika ambapo kuna ujenzi wa mabweni 4 ya wafungwa yenye uwezo wa kuhifadhi wafungwa 50 kila moja, uvutaji wa maji na ujenzi wa mabweni 2 ya wanawake.Kazi zinazoendelea ni ujenzi wa jengo la utawala, nyumba za watumishi.

Share it:

habari

Post A Comment: