Serikali Mkoani Geita,imesema kuwa Haina tatizo na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) na kwamba
haiwezi kuendelea kukubali jambo baya ambalo linafanywa na mtu mmoja kuchafua
sura ya mgodi mzima kwani shughuli
ambazo zimeendelea kufanywa zimeendelea kuleta manufaa kwa Taifa na mkoa kwa
ujumla.
Akizungumza baada ya ziara yake ya kutembelea na kuona namna
ambavyo mgodi huo umekuwa ukifanya shughuli za uzalishaji wa dhahabu,Mkuu wa
mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema
mgodi na serikali ni kitu kimoja
kutokana na kwamba wamekuwa wakilipa fedha kwa Taifa pasipo kuwa na udanganyifu
wa aina yoyote.
“Hatuwezi tukakubali jambo lolote lile likafanywa na mtu
moja likaonekana uongozi wa mgodi na serikali kwamba hatuna mahusiano mazuri
mimi napinga kwa nguvu zote mgodi na serikali tuko kitu kimoja hawa ni
wawekezaji wazuri wanalipa fedha zinazotakiwa kwa wakati na kama kuna
changamoto chache chache zinaelezeka tukae pamoja tutatue”Alisema Luhumbi.
Kuhusu miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa na mgodi
huo,Luhumbi alisema kuna makosa mengi ambayo yalifanyika kwa miaka ya
nyuma kutokana na miradi ambayo ilikuwa ikipangwa wananchi walikuwa hawafahamu
na kwamba kutokana na timu ambayo imewekwa kwa sasa ya mgodi wanaamini miradi ambayo imepangwa itatekelezwa kwa haraka
na kwa wakati zaidi.
“Makosa mengi yalifanyika katika miradi ya nyumba kosa moja
ambalo lilifanyika wewe huwezi kupanga mradi bila ya wananchi kuwa tayari
wanafahamu huo mradi na kuna maandalizi mazuri lakini kwa timu ambayo
imetengenezwa kwa wakati huu wakurugenzi wote wameshakaa na wamepitisha kwenye
vikao halali vya halmashauri kwa hiyo
hili jambo lipo kisheria sana hapa tulipo kuna hatua moja ambayo imebakia ya
kuweka sahihi ili miradi ianze kutekelezwa”alisema Luhumbi.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi
amesikitishwa na kitendo cha mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) kuandika barua kwa
viongozi wa makanisa ya Romani na AIC kukataza fedha za maendeleo kupelekwa
kwenye miradi suala ambalo sio kweli kutokana na sheria ya mwaka 2017
kubadilishwa ndio chanzo ambacho kinapelekea fedha kujadiliwa na halmashauri husika.
Aidha Meneja mahusiano huo
Tenga B Tenga alisema lengo la
mgodi ni kuhakikisha wananchi ambao wanauzunguka wananufaika nao kwa nyanja
mbali mbali zikiwemo za afya,uchumi pamoja na Elimu.
Post A Comment: